Wednesday, October 28, 2020

YOTE TISA, KUMI WALE KEPU VEDE UBWABWA WATAITA UWAWA BAADA YA GEMU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

DOMO LA MFUA JEZI

IYENA iyeeena… iyeeeena iyeeeena Mfua jezi nambari wani. Tuimbe wote sasa iyeeena iyeeena Mjezinho hana mpinzani. Teh teh teh mijezi oyeeee… mibukta oyeeee… mibipsi oyeeee… misoksi oyeeee.

Bado mi naendelea kutoa salamu asee… Manula oyeeee… Samatta wetu oyeee…. Kwa hapa sasa ngoja nitoe salamu kwa heshima zote. Mashabiki wa Stazi oyeeee… teh teh teh Kepu Vede wanatokea wapi sasa?

Inawezekana hata mlango walioingilia wasiujue sembuse wa kutokea? Kudadadeki kazi wanayo hao shombe shombe, kipigo hakiepukiki kabisa kwao, wataisoma namba leo.

Haloooo Amunike, najua umesikia na kuona kilio cha Watanzania asee.. sisi mashabiki woteee tupo nyuma yako na timu, sasa cha kufanya kazi kwenu kutupa raha tu siku ya leo.

Unajua kabla ya mbugi kupigwa, rafiki yangu mmoja alinambia eti Mjezinho hao Shombe shombe ni tawi la Ureno? Jamaa alinishawishi weeee, mpaka nikaanza kuamini, lakini leo hakuna cha tawi wala nini hata wangekuja na Kristiano Ronado wangepigwa tu.

Vigezo vyake sasa. Eti waliwahi kuwa koloni la Ureno, sijui kipa wao aliwahi kuwa huko ligi ya Ureno sijui, sasa kazi wanayo inabidi wajue hata sisi tunaweza kumshusha Hari Kane hapa Bongo wakati wowote, kwa hiyo bora wasalimu amri mapema tu.

Teh teh teh salamu bado zinaendelea asee, haziwezi kuisha juu kwa juu hizi. Msuva oyeeee… Yule Bocco naye nampa salamu tu… Mudathir oyeeee maana hiyo miguu yako kama kipima maji kinavyoweza kunyoosha mipasi asee.

Niendelee ama nisiendeleee, watu bhana eti endelea tu Mjezinho basi ngoja nitoe salamu kwa watu kedekede sababu hizi salamu haziwezi kuisha asee, yaani kama kwenye matangazo ya redio vile. Yondani oyeeee…. Sasa kujua kama mchezo umeisha mapema Amunike si kamwita na yule beki mwenye akili kama zote, makofi kwa Nyoni tafadhali.. teh teh teh Kepu Vede wasije kususa kuingia uwanjani tu maana hao watu waliopo Stazi ni motoooo.

Ile ni roho ya kikatili sana, huwezi kuwa vile na roho ya mnyama asee. Unadhani Amunike ametumia ubinadamu kumwita Nyoni asee, ngoja nisiendelee kuwatisha wageni wetu wanaweza kususa na kula kabisaaaa, wakafa kwa mawazo.

Kapombe oyeee, yaani hapa najaribu kumrudishia meseji yule aliyeniambia siku ile kuwa hawa Kepu Vede ni tawi la Ureno, lakini kama wangekuwa tawi kweli si wangeazima watu huko kwenye koloni lao.

Salamu yangu imebaki moja. Bado namtafuta wakumpa, acha niendelee kukupa ubuyu kabla sijafunga salamu zangu asee. Hivi kama yule Himid Mao akiamua kucheza kininja kweli si watakufa nyingi jamani.

Hatuwezi kukubali kilichotokea, labda mchezo wetu utachezwa leo jioni lakini sio ule wa kule kwao ambao walijidai wenyewe. Sasa salamu yangu ya mwisho inaenda kwa Kepe Vede oyeeee, yaani nyie bhana kaeni mjue mna kazi ngumu sana saivi.

Yaani Kepu Vede hawakujua kama kutufunga vile tulikuwa na maana yetu, teh teh teh wameanzisha ugomvi wa mawe halafu wanaishi katika nyumba ya vioo, sasa watalala nje wake wakijua hilo na hili joto la Das’lamu hapa watajibeba.

Kilichobaki sasa ni kufanya umafia tu, kwanza gari la lazima lipitie ruti ya Ubungo kwenye foleni, wakae weeeee mpaka wafike uwanjani miguu yote imelegea, kudadadeki yaani heri wasuse kucheza kuliko kujipendekeza kuingia uwanjani, maana ule ubwabwa watauita uwawa, kazi wanayo hao shombe shombe.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -