Friday, October 30, 2020

ZAHERA ABARIKI NENDA RUDI WACHEZAJI STARS

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI            |               


 

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amebariki ratiba ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza utaratibu wa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Taifa Stars kuruhusiwa kwenda kuzitumikia klabu zao kwenye mechi za Ligi na baadaye kurudi tena katika timu ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alipokuwa akizungumza na wanahabari jana, ambako alisema kuwa, Zahera ameondoka kwenda kuungana na timu ya Taifa Kongo (DRC), lakini amebariki utaratibu huo uliowekwa na TFF.

Alisema kutokana na ratiba ya Ligi kuingiliana na kambi ya Stars, hawana budi kukubali utaratibu huo kwa ajili ya kuendelea kuwapata wachezaji wao kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

“Ilikuwepo taarifa ya mapema kuhusu utaratibu wa kuwaruhusu wachezaji waliopo Stars kurudi kuzitumikia timu zao, mwalimu hana shaka na suala hilo, yeye ameondoka leo (jana) kwenda kwenye majukumu yake na timu ya Taifa ya Kongo, timu itakuwa chini ya Kocha Noel Mwandila,” alisema Ten.

Katika hatua nyingine, uongozi wa klabu hiyo umeanza mikakati yake kwa ajili ya mechi zao za mikoani, ambako tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu, timu hiyo imecheza mechi zake mfululizo nyumbani.

Akizungumzia hilo, Ten alisema, katika kuhakikisha timu yao inapata matokeo mazuri mikoani, tayari mipango hiyo imeanza na wamekutana na viongozi mbalimbali kutoka mikoa ya Mbeya, Mwanza na Kilimanjaro kwa ajili ya kujenga umoja wao.

“Tunafahamu kuwa mechi za mikoani zina changamoto nyingi, tunahitaji ushindi tunaouapa sasa tukiwa nyumbani basi na ugenini ikawe hivyo, ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi kwa mara ya 28,” alisema Ten.

Yanga imeshacheza mechi tano nyumbani, huku ratiba ya michuano hiyo ikionyesha wana mechi nyingine sita zaidi wakiendelea kusalia, timu hiyo inatarajia kuanza mechi za mikoani Novemba 25, dhidi ya Kagera Sugar, Kaitaba Kagera.

Mechi nyingine ni dhidi ya Tanzania Prisons Desemba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Desemba 29 dhidi ya Mbeya City, mkoani humo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -