Wednesday, October 21, 2020

ZAHERA ACHIMBA MKWARA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

*Ataka wachezaji wanaowaza kufungwa na Simba wabaki nyumbani

*Tshishimbi amjibu kibabe

NA ZAITUNI KIBWANA, MOROGORO


BAADA ya kufanya mazoezi ya nguvu na kucheza mechi tatu za kujipima nguvu, kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewachimba mkwara wachezaji wake akiwataka wanaodhani watafungwa na Simba wabaki nyumbani.

Tayari Yanga imecheza mechi dhidi ya Mawezi Market na kushinda bao 1-0, Kilosa Kombaini ikashinda tena 1-0 na jana ilijitupa uwanjani dhidi ya Mkamba Rangers Morogoro.

Kocha huyo mwenye ‘confidence zake mjini’, ametamba kuwa hatishiki na majina makubwa ya wachezaji wa Simba waliosajiliwa msimu huu, kwani mpira hauchezwi na majina.

Simba imemsajili nyota wa Rwanda mwenye asili ya Kiganda, Meddie Kagere, ambaye alikuwa moto wa kuotea mbali katika michuano ya Sportpesa Super Cup akiwa na Gor Mahia ya Kenya, mwingine ni nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Zambia, Cletus Chama Chota, Hassan Dilunga, Paschal Wawa, Adam Salamba na Mohamed Rashid.

Lakini Zahera akizungumza na BINGWA jana kwenye kambi ya Yanga iliyopo Morogoro na kusema kuwa kikosi hicho kipo tayari kucheza na timu yoyote ile.

“Mpira ungekuwa unachezwa na majina basi Brazil ingebeba Kombe la Dunia, ila majina hayachezi mpira hata uwe na nani na nani ukishaingia uwanjani tu wote wanakuwa ni wachezaji, hivyo hatuhofii majina yao tupo tayari kucheza na yeyote yule,” alisema.

“Kuna wachezaji wameanza kujilalamisha eti Simba sijui nini wazuri, mara watatufunga, sasa nawaambia ikifika hiyo siku ni bora wabaki nyumbani na wasiangalie mpira kwenye televisheni wasubiri dakika 90 za mchezo,” alisema Zahera.

“Si wachezaji pekee, hata shabiki anayewaza kuwa tutafungwa nawaambiwa wabaki nyumbani, wasije kabisa uwanjani kwani sisi hatuangalii tunacheza na nani,” alisema.

Zahera alisema kikosi hicho kwa sasa kina ujasiri wa hali ya juu wa kupambana na timu yoyote.

“Si Simba tu, tupo tayari kucheza na yeyote yule, awe mkubwa au mdogo kwa sababu tunajiamini kutokana na mazoezi tuliyofanya,” alisema.

Yanga inatarajia kurejea Dar es Salaam kesho kwa ajili ya mchezo wao dhidi USM Alger, utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakuwa ni wa kukamilisha ratiba kutokana na kuburuza mkia katika Kundi D la michuano hiyo wakiwa na pointi moja, huku Gor Mahia wakiongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao wakiwa sawa kwa pointi nane na USM Alger na Rayon Sports wakishika nafasi ya tatu kwa pointi tatu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -