Monday, October 26, 2020

ZAHERA AFICHUA SIRI YANGA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SAADA SALIM


HATIMAYE siri ya Kocha Mkuu wa Yanga, `Papa`, Zahera Mwinyi kushindwa kukaa katika benchi imefichuka kuwa ni kutokana na kukosa kibali cha kufanyia kazi nchini.

Zahera aliwasili nchini mwishoni mwa msimu uliopita, kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha George Lwandamina ambaye alirejea kwao Zambia kuungana na timu yake ya zamani Zesco United.

Hivi karibuni uongozi wa klabu hiyo ulidai kwamba kibali cha kocha huyo kipo tayari na kinachokwamisha ni suala lingine ambalo liko kwenye utawala na wanalifanyia kazi.

Lakini tangu Zahera awasili nchini mpaka sasa hajapatiwa kibali cha kufanyia kazi nchini na ndio maana bado anaendelea kukaa jukwaaani wakati wa mechi za timu hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana kwa njia ya mtandao akiwa kwao DR Congo, Zahera, alisema hana vibali vya kufanyia kazi ndio sababu ya kushindwa kukaa katika benchi la ufundi la timu hiyo.

“Sikai benchi kutokana na kukosa kibali cha kufanyia kazi, lakini nitaungana nao kwenda Rwanda kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports,” alisema Zahera.

Mchezo huo wa Kundi D kati ya Rayon na Yanga unatarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Amavibi mjini Kigali, ukiwa ni mtanange wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Baada ya mechi hiyo kocha huyo, Zahera alisema ataungana na timu yake ya Taifa ya DR Congo, ambayo wanatarajiwa kucheza mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Liberia itakayochezwa Septemba 7, mwaka huu.

“Nitakuwa na timu baada ya mechi siku ya Jumatano nitaondoka kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Congo, pia sitakuwapo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC, lakini program zote zitakuwa chini ya msaidizi wangu Noel Mwandila,” alisema Zahera.

Alisema tayari ameshakabidhi mafaili ya program zake kwa Noel, hivyo mashabiki wasiwe na hofu juu ya kutakuwapo kwake katika kipindi atakachokuwa na majukumu ya timu ya taifa.

Uongozi wa Yanga kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Hussein Nyika, aliliambia BINGWA kuwa bado anapambania kibali cha Zahera.
Nyika alisema mpaka sasa kibali cha kazi nchini ambacho Zahera anapaswa kuwa nacho hakijapatikana, hivyo juhudi zinaendelea ili kufanikisha na hatimaye awe anakaa kwenye bechi la ufundi wakati wa mechi.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa kibali hicho kitapatikana kwa kushirikiana na serikali na mpaka sasa wanaendelea kupambana ili kiweze kupatikana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -