Monday, October 26, 2020

ZAHERA AJA JUU KISA AJIB

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA TIMA SIKILO


 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewaomba mashabiki kuacha kuumizwa na kitendo chake cha kumtoa mapema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Ajib, kwani yeye kama mwalimu aliona anafaa kufanyiwa mabadiliko walipovaana na Stand United juzi.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga ilishinda mabao 4-3.

Hata hivyo, mashabiki wa Yanga hawakuwa na furaha na ushindi huo kutokana na timu yao kuruhusu kufungwa mabao matatu, mawili yakipatikana baada ya kutolewa kwa Ajib na Mrisho Ngassa.

Ajib alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioifungia Yanga kabla ya kutolewa katika dakika ya 55 kumpisha Yusuph Mhilu, huku mabao mengine yakiwekwa kimiani na Ngassa, Vincent Andrew ‘Dante’ na Kaseke.

Akizungumza na BINGWA jana, Zahera alisema Ajib ni mchezaji mzuri, lakini hiyo si sababu ya kumfanya acheze mwanzo mwisho ukizingatia kuwa alishachoka baada ya kutumia nguvu nyingi muda wote aliokuwapo uwanjani.

“Ajib aliipatia timu bao moja lakini hiyo haikuwa sababu ya kufanya aendelee kucheza dakika zote 90, kwani alikuwa tayari ameshachoka hivyo ilikuwa ni busara kumfanyia mabadiliko,” alisema Zahera.

Alisema bado wana michezo mingi mbele hivyo ana imani kama wachezaji wataendelea kujituma kwa nguvu zao bila kuangalia changamoto zinazowakabili, watafanya vizuri zaidi.

Mchezo huo wa juzi ulikuwa ni wa pili Kwa Yanga baada ya awali kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwa ushindi huo, Yanga wamefikisha pointi sita, wakiwa na mabao sita ya kufunga na kufungwa manne, huku timu hiyo ikiwa nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -