Saturday, October 31, 2020

ZAHERA AMKATAA CHIRWA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA TIMA SIKILO

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amemkataa Obrey Chirwa ndani ya kikosi chake, akidai kuwa mshambuliaji huyo hafai kwani si mtu wa kujitolea wakati wa matatizo.

Chirwa aliitumikia Yanga kwa misimu miwili akitokea nchini Zambia na mara baada ya kumaliza mkataba wake msimu uliopita, alitimka na kwenda kucheza soka katika kikosi cha Ismailia ya nchini Misri.

Msimu uliopita, Chirwa aliwahi kugoma kukitumikia kikosi cha Yanga kutokana na kutolipwa mshahara wake wa miezi mitatu na kwamba mkataba wake ulipomalizika, aliachana na Wanajangwani hao.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Zahera alikiri kuwa Chirwa si mchezaji mbaya, lakini hawezi kumrudisha ndani ya kikosi chake kutokana na tabia zake mbaya za kukataa kuisaidia timu wakati inahitaji msaada wake.

Alisema ni michezo mingi ambayo mshambuliaji huyo alikataa kushiriki, ukiwamo ule wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger nchini Algeria na mingineyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo kwa kukosekana kwake, kuliiathiri sana Yanga na kujikuta ikipokwa ubingwa wao wa ligi hiyo.

“Nasikia watu wanasema Chirwa amerudi Yanga. Mimi kama kocha mkuu, nasema mchezaji huyo alitupatia matatizo sana wakati timu ikiwa ina hali ngumu, huku akiwa na kazi kubwa ya kuisaidia timu, lakini alikataa michezo isiyopungua mitano.

“Kama nitamrudisha tena wakati hawezi kujitolea klabu inapokuwa na shida, nawezaje kufanya naye kazi? Alikuwa akikataa kufanya mazoezi, timu ilisafiri Algeria bila yeye pamoja na kwenda mikoani katika michezo mbalimbali ya ligi alikataa, siwezi kumrudisha kwenye timu yangu,” alisema Zahera.

Alisema Chirwa aliwahi kugomea mazoezi kwa sababu ya madai yake hayo, huku akimshangaa kufanya hivyo wakati hakuwa akidai peke yake.

Chirwa alikuwapo uwanjani juzi wakati Yanga ikivaana na Alliance ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao Wanajangwani hao walishinda mabao 3-0.

Habari zilizopatikana uwanjani hapo, zinadai kuwa Mzambia huyo yupo njiani kutua Yanga kipindi cha dirisha dogo la usajili, baada ya kuachana na Ismailia.

Katika hatua nyingine, Zahera amewafunga mdomo wale wote wanaomkosoa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, kwa kutomwita mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib, akisisitiza hata kama angekuwa ni yeye, angeachana naye.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Zahera, alisema japo Ajib ni mchezaji mzuri, lakini hana uwezo wa kupambana kwa dakika zote 90 kwa kasi ile ile.

“Ajib ni mchezaji mwenye akili ya mpira kuliko wachezaji wote wa timu ambazo nimewahi kucheza nazo hapa Tanzania, anacheza huku akijua mbele kitatokea nini, hakuna anayeweza kumfikia, lakini hata kama ni mimi ndio kocha wa timu ya Taifa, kwa uwezo aliouonyesha uwanjani, nisingeweza kumwita katika kikosi changu,” alisema.

Alisema ili Ajib acheze katika timu ya Taifa, anahitaji kuongeza juhudi zaidi kwani wachezaji wa timu inayowakilisha nchi, wanahitaji kujitolea zaidi na kujituma kwa kiwango cha hali ya juu

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -