Tuesday, October 27, 2020

Zahera amkataa Chirwa

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga,Mwinyi Zahera amesema hana mpango wa kumsajili mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Mzambia Obrey Chirwa kwakua hana uvumilivu pale timu inapokua na shida.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumapili Oktoba 22, Zahera amesema amesikia tetesi kutoka kwa watu kwamba Yanga ina mpango wa kumsajili Chirwa  aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita 2017/18 na kuelekea timu ya Nogotoom ya Nchini Misri.

“Nimesikia watu wanasema kwamba Chirwa amerudi Yanga, Kama mimi ndiye kocha wa Yanga Chirwa hatorudi pale, aliipatia timu matatizo ilipokua haina kitu, alikataa kucheza baadhi ya mechi kwasababu hajalipwa mshahara, hadi mazoezi alikataa kufanya.

“Timu imesafiri kucheza mechi nyingi hadi ya kimataifa na Algeria bila yeye wakati alikua akijua kabisa anategemewa, mimi Zahera mchezaji wa namna hii siwezi kumsajili katika timu yangu, ” amesema Zahera.

Tetesi za kurudi Chirwa katika kikosi cha Yanga zimeanza kusikikajanan baada ya mchezaji huyo kuonekana uwanja wa taifa akishuhudia timu yake ya zamani Yanga ikimenyana na Alliance ya Mwanza mchezo uliomalizika kwa Yanga Kushinda magoli 3-0.

Chirwa alionekana akiwa amekaa meza moja na baadhi ya Viongozi wa Yanga, Mwenyekiti wa kamati ya Usajili, Hussein Nyika na Kaimu katibu wa Klabu hiyo Omary Kaya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -