Saturday, October 31, 2020

ZAHERA AMUUZIA KESI TAMBWE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR


KOCHA wa Yanga, Zahera Mwinyi, amemuuzia kesi mshambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe, kutokana na kuchoshwa na maswali ya mashabiki ambao hawajui kwanini hapangwi, wakimtaka kocha huyo aweke mambo sawa ili Mrundi huyo aanze kukinukisha.

Akizungumza na BINGWA akiwa Rwanda mapema jana, Zahera alisema hana majibu ya moja kwa moja kuhusu kutompanga Tambwe, ingawa kocha huyo alishawahi kusema kuwa mfumo anaoutumia ndio uliofanya kumweka kando nyota huyo.

“Hilo swali naulizwa sana, mpigieni simu yeye (Tambwe) kisha muulizeni sababu, lakini mimi sina jibu,’’ alisema Zahera.

BINGWA lilimtafuta Tambwe na kumuuliza sababu za yeye kutopata nafasi, ambapo alisema yupo fiti na hajui sababu hasa za yeye kutochezeshwa katika kikosi cha kwanza, lakini akiamini ipo siku atarudi katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

“Mimi nipo fiti, sina majeraha. Kuhusu kucheza au kutocheza, hilo ni suala la kocha, lakini sisumbuliwi na chochote na ninaendelea kupambana kadri ya uwezo ili kumshawishi anipe nafasi,” alisema Tambwe.

Mapema wiki iliyopita, Zahera alikaririwa na kudai kuwa Mrundi huyo yupo fiti, ila mfumo anaoutumia ndio umekuwa kikwazo cha yeye kutomtumia.

Alisema nafasi anayocheza Tambwe kwa sasa inashikiliwa na wachezaji ambao wanamshawishi kuwapa nafasi kila mara, hivyo suala la kwamba ni mgonjwa, si kweli.

Tambwe aliwahi kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, wakati huo akiichezea Simba na hata alipotua Yanga aliuwasha moto kisawasawa na kubeba kiatu cha dhahabu.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -