Friday, October 30, 2020

ZAHERA: ANAYEKUJA NA AJE TU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

BAADA ya Yanga kutoa dozi ya mabao 2-0 dhidi ya Singida United jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha wa kikosi hicho Mwiny Zahera amejitamba kwamba yuko tayari kuvaana na mahasimu wao Simba.

Huo ni mchezo wa nne mfululizo kwa Yanga kutoa dozi katika mechi za Ligi Kuu na kumpa kocha wao matumaini ya kuivaa Simba Jumapili hii.

Mchezo huo wa jana ambao ulianza kwa timu zote kusoma katika dakika za mwanzo, kabla ya nyota wa Singida United, Amara Diaby kupoteza nafasi dakika 19 akishindwa kumalizia pasi nzuri ya Geofrey Mwashiuya kwa kupiga shuti kubwa lililotoka nje.

Dakika ya 25 Feisal Salum ‘Fei Toto’alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Daniel Warioba kutoka Mwnaza kwa kumchezea rafu Kenny Ally.

Mshambuliaji wa Burundi, Amis Tambwe aliwaamsha mashabiki wa Yanga majukwani kwa kufunga bao zuri kwa kichwa dakika ya 29, akiunganisha majalo ya Ibrahim Ajib.

Ajib aliikosesha Yanga bao lingine dakika ya 39, kutokana na mpira uliorudishwa na mlinda mlango wa Singida, Robert David na kuuwahi mpira huo na ‘kuuchop’ lakini ukapaa juu ya goli.

Singida walikaribia kusawazisha dakika ya 42, baada ya mpira wa kona uliopigwa na Athanas Mdamu na Elisha Muroiwa kupiga kichwa kilichookolewa na kipa wa Yanga, Ben Kakolanya.

Dakika moja baadaye Singida walikosa tena bao baada ya kona ya Kenny Ally kugonga mwamba na kuokolewa na mabeki wa Yanga.

Yanga waliandika bao la pili dakika 45 likifungwa tena na Tambwe akiunganisha pasi ya Gadiel Michael na kumfanya nyota huyo kuwa na mabao mawili msimu huu katika mechi mbili alizocheza.

Yanga walikwenda mapumziko wakiw mbele kwa mabao hayo 2-0 na kipindi cha pili kuanza kwa Diaby kuonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Papy Tshishimbi dakika ya 48.

Singida walifanya mabadiliko dakika ya 54 kwa kumtoa Mwashiuya na Mdamu ambao nafasi zao zilichukuliwa Awesu Awesu na Habibu Kiyombo.

Nao Yanga walifanya mabadiliko dakika ya 79 kwa kumtoa Deus Kaseke na kuingia Juma Makapu na wakati huo huo Matheo Antony alipoteza nafasi baada kupewa pasi nzuri na Ajib, lakini shuti lake likapaa angani.

Yanga walifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Tambwe na kuingia Yusuph Mhilu dakika ya 84.

Lakini mabadiliko hayo hayakusaidia timu zote mbili kubadilisha matokeo hayo na dakika 90 kumalizika kwa Yanga wakiibuka kidedea kwa mabao hayo 2-0.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -