Wednesday, October 28, 2020

ZAHERA BONGE LA MAFIA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU


*Awavuta Yanga mastraika wawili, beki hatari wa DR Congo

*Asema akiwapata, hakuna ‘paka’ yeyote wa kuisumbua Yanga 2018/19

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amekiangalia kikosi chake na kubaini kinahitaji kuongezewa nguvu na hivyo kupiga hodi ndani ya timu ya Taifa lake, DR Congo na kufanikiwa kupata vifaa vya maana.

Zahera alikuwa na kikosi cha DR Congo tangu wiki iliyopita kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Liberia kwenye Uwanja wa Samuel Kanyon Doe Sports, mjini Monrovia jana.

Mchezo huo uliopangwa kuanza saa 1:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ulikuwa ni muhimu mno kwa DR Congo kwani ushindi ungeiwezesha kuongoza Kundi D kwa kufikisha pointi sita.

Akizungumza na BINGWA juzi, Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa DR Congo, alisema kuna wachezaji waliopo katika kikosi hicho cha nchi yake ambao anaamini wakitua Yanga, hakuna timu itakayowasumbua Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Katika timu ya Taifa ya DRC, kuna starika wazuri sana na hata mabeki, lakini wote wanacheza nje ya Congo, wapo wanaotoka Ulaya na timu nyinginezo za Afrika.

“Nimezungumza na wachezaji wengi tu ili waje Yanga, lakini tatizo ni mishahara yao, wapo wanaolipwa zaidi ya euro 50,000 (Sh mil 130) na wengine wanaocheza TP Mazembe au Vita Club ni kati ya USD 5,000 (Sh mil 11) na 8,000 (Sh mil 18) au chini ya hapo. Sasa kwa mishahara hiyo ni vigumu kukubali kuja Yanga,” alisema Zahera.

Alisema iwapo atajitokeza mtu Yanga kuwa tayari kutoa fedha, ana uwezo wa kuiletea timu hiyo wachezaji wa kiwango cha juu wa idara zote, kuanzia mabeki, viungo na hata washambuliaji.

Aliwataja wachezaji waliopo DR Congo ambao wapo tayari kutua Yanga iwapo Wanajangwani hao watafika bei kuwa ni washambuliaji, Ben Malango na Elia Meschak (TP Mazembe), Cedric Kilua (SM Sanga Balende) na beki Ngonda Muzinga (Vita Club) na wengineo wengi.

Kikosi cha Yanga cha sasa kina mshambuliaji mmoja tu wa kiwango cha juu ambaye ni Herieter Makambo kutoka DRC, huku Matheo Anthony akiwa bado hajawateka mashabiki wa timu hiyo kama ilivyo kwa kinda Yusuph Mhilu, Pius Buswita na Emmanuel Martin.

Kwa upande wa viungo washambuliaji, kuna Ibrahim Ajib, Mrisho Ngassa na Deus Kaseke, huku viungo wakiwa ni Feisal Salum ‘Fei Toto’, Pappy Tshishimbi (DRC), Said Juma Makapu, Rafael Daudi, Said Mussa na Maka Edward.

Katika safu ya ulinzi, Yanga ipo vizuri katikati japo nako kunahitaji kuongezewa nguvu kama ilivyo upande wa kulia na kushoto.

Yanga ilishindwa kufanya usajili wa kishindo baada ya kumalizika kwa msimu uliopita kutokana na wimbi la ukata linalowakabili ambapo kwa sasa mashabiki na wanachama wamekuwa wakisubiri kwa hamu Uchaguzi Mkuu kuona iwapo watapata viongozi watakaokuwa na ushawishi wa kuyavuta mataji zaidi Jangwani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -