Wednesday, October 28, 2020

ZAHERA: MVUA IMECHANGIA KIPIGO RWANDA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA


KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amelalamikia hali ya hewa ya mvua iliyokuwa nchini Rwanda, kuwa imechangia kupoteza mchezo wao wa juzi dhidi ya Rayon Sports.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika wa kundi D, ulichezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo Kigali, nchini Rwanda na Yanga kufungwa bao 1-0 na wenyeji Rayon Sports.

Akizungumzia mchezo huo, Zahera alisema mchezo huo ulikuwa mgumu kutokana na mvua iliyonyesha kuanzia asubuhi mpaka wanaingia katika uwanja huo.

“Ilikuwa kazi kwa wachezaji wangu, mvua ilinyesha mwanzo wa mechi mpaka mwisho na kufanya mchezo uwe mgumu na uwanja ulijaa maji, wachezaji walikua wanateleza tu,” alisema.

Zahera aliyerithi mikoba ya Mzambia, George Lwandamina, alisema mbali na mvua waamuzi wa mchezo huo hawakutumia vema sheria 17 za soka.

Sisi tulikuwa kumi na moja lakini wapinzani wetu walikuwa 14, mwamuzi alikuwa upande wao na mashabiki kutokana na kuwa nyumbani,” alisema Zahera.

Alieleza kikosi hicho kitarejea leo na kupumzika, kabla ya kesho kuingia kambini kujiandaa na michezo inayofuata.

“Tutaanza mazoezi kujiandaa na safari ya mkoani Kigoma kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United, Septemba 5 mechi itakayochezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika,” alisema Zahera.

Yanga SC wamekamilisha mechi zao za Kundi D na kuburuza mkia wakiwa na pointi nne, nyuma ya Gor Mahia yenye pointi nane na kushindwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Kwa matokeo ya juzi, Rayon inasonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili ikijikusanyia pointi tisa, nyuma ya USM Alger yenye pointi 11 baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya.

Yanga SC sasa wanarejea nyumbani Tanzania kuelekeza nguvu zao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu kwani mwakani hawatashiriki tena michuano ya Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -