Wednesday, November 25, 2020

ZANACO KUMNG’OA MSUVA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

KIWANGO cha winga wa Yanga, Simon Msuva, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kimemkuna kocha wa Zanaco ya Zambia, Numba Mumamba na imeonekana wazi kwamba hatakuwa na maisha marefu kwenye kikosi hicho cha Jangwani.

Mumamba amesema amekiangalia kikosi hicho cha Yanga na kusema ni Msuva pekee ambaye alifunga bao katika sare ya 1-1 ndiye anayeweza kuwasumbua katika mchezo wa marudiano utakaopigwa  Jumamosi ijayo mjini Lusaka, Zambia.

Kocha huyo amesema Msuva ni mtu hatari ambaye anatakiwa kuwekewa ulinzi wa kutosha kwenye mchezo wa marudiano ili asiweze kuleta madhara tena kama ilivyokuwa kwenye mechi ya kwanza.

Akizungumza na BINGWA, Mumamba alisema alikuwa anakifahamu vyema kikosi chote cha Yanga baada ya kuwaona kupitia kwenye CD, lakini ni Msuva pekee ambaye anaweza kuwa na madhara kwao.

“Yule aliyevaa namba 27 ni hatari sana tena sana, ana kasi sana. Ni mtu ambaye anaweza kuleta madhara muda wowote langoni mwako, pia anaweza kuamua matokeo ya mchezo, ni lazima tujipange kisawasawa,” aliongeza Mumamba.

 

Alipoulizwa kama wanaweza kumng’oa winga huyo kumjumuisha kwenye kikosi chake kama wakisonga mbele kwenye michuano hiyo, Mumamba alisema atakaa na uongozi wake kuangalia uwezekano huo wa kunasa saini ya msuva.

“Yule (Msuva) ni mchezaji mzuri sana. Tunaweza kuangalia namna ya kufanya juu yake, anaweza akatufaa kwenye kikosi chetu, hasa tukivuka hatua za mbele,” alisema Mumamba.

Msuva kwa sasa anaongoza kwa mabao Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwa amepachika jumla ya mabao 12, wakati kwenye michuano ya kimataifa ambayo klabu yake imeshiriki hadi sasa, ametingisha nyavu mara 19.

Pia kocha huyo alisema kuwa ana uhakika mkubwa wa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Machi 18, mwaka huu kwani anarudi Zambia kwenda kufanyia kazi mapungufu yote aliyoyaona katika mchezo wa kwanza.

“Yanga wana mapungufu mengi sana, hawajajipanga wala hawachezi kitimu, pia hawana stamina. Mambo mengine siwezi kukwambia ila elewa kwamba tumeshamaliza kazi hapa kwao,” alisema Mumamba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -