Tuesday, December 1, 2020

ZANACO WATAENDELEZA MAJANGA YA YANGA KIMATAIFA?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

IMEBAKI wiki moja kabla ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kuwavaa Zanaco maarufu kwa jina la ‘Bankers’ kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga watawavaa Zanaco kwenye mchezo huo kuwatoa Ngaya de Mbe ya Comoro kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-2.

Mchezo wa kwanza utachezwa Machi 11 kwenye Uwanja wa Taifa na kisha baadaye timu hizo zitakutana Zambia kumaliza kazi.

Mabingwa hao wa Zambia wanakutana na Yanga ikiwa ni baada ya kuwaondoa APR ya Rwanda katika raundi ya kwanza.

Zanaco walipita kwa ushindi wa bao 1-0 baada ya kupata matokeo ya kutofungana mjini Lusaka na kabla ya kupata ushindi wa bao 1-0 wakiwa ugenini.

Kimsingi kuelekea katika mchezo huo wa Machi 11, Yanga wanatakiwa kuwa makini kutokana na ukweli kwamba Zanaco si timu ya kubeza hata kidogo kama washabiki na wapenzi wengi wa soka hapa nchini wanavyofikiri.

Historia yao Zambia

Zanaco ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Zambia, si miongoni mwa klabu kongwe barani Afrika ikiwa na umri wa miaka 32 tu ikianzishwa rasmi mwaka 1985.

Zanaco ilianzishwa na Benki ya Biashara nchini Zambia (NBC) ikiwa ni timu ya wafanyakazi wa taasisi hiyo na ndilo chimbuko la jina Bankers.

Umri wa Zanaco ni tofauti na wapinzani wao Yanga SC ambao Februari 11 mwaka huu walitimiza miaka 82 toka kuanzishwa kwake mwaka 1935.

Zanaco ni miongoni mwa timu zenye mafanikio makubwa nchini Zambia kutokana na uongozi wake kuwa imara hususani masuala ya kiuchumi.

Ubora katika utendaji umewafanya kumiliki uwanja wao unaoitwa Sunset wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.

Mafanikio yao ya uwanjani ni pamoja na kuchukua vikombe saba vya Ligi Kuu Zambia, vinne vya Ngao ya Jamii na moja la Kombe la Cocacola.

Lakini pia, wakali hao wa Lusaka wameshinda mara moja Kombe la Mei Mosi na kunyakua mara moja Kombe la Shirika la Mafuta la BP.

Wakiwa wamefanya hivyo mara saba, Zanaco ni timu ya tatu kuchukua mara nyingi taji la Ligi Kuu Zambia, wakiwa nyuma ya Nkana (12) na Mufurila Wanderers (9).

Rekodi yao Ligi ya Mabingwa Afrika

Katika ngazi ya michuano ya kimataifa, kwa mara ya kwanza Zanaco FC ilishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003, lakini waliondoshwa katika hatua ya kwanza.

Historia yao nzuri kwenye mashindano hayo ni ile waliyoiweka mwaka 2010 kwa kufika hatua ya 16 bora.

Walipotolewa katika hatua hiyo, waliangukia Kombe la Shirikisho na kuishia hatua ya makundi.

Licha ya uchanga wake kulinganisha na Yanga, lakini rekodi zao kimataifa hazipishani kwa kiasi kikubwa.

‘Uchawi’ wao ni makocha, wachezaji wazawa

Moja ya sifa kubwa ya timu hii ni kutumia makocha wazawa. Haijawahi kutumia makocha kutoka nje ya Zambia. Hiyo imewapa sifa ya uzalendo na kutoa fursa kwa wazawa kuonesha uwezo wao kuinoa klabu hiyo kubwa barani Afrika.

Ukiondoa suala la kutumia walimu wazawa katika kikosi chao cha wachezaji 30, ni wawili tu kutoka nje ya Zambia. Wanaye kiungo mshambuliaji raia wa Chile, Leiva Garcia na kiungo Atram Kwame kutoka Ghana.

Kwa sasa Zanaco wananolewa na mchezaji wao wa zamani ambaye ni swahiba mkubwa wa kocha George Lwandamina wa Yanga, Mumamba Numba ‘Black Mamba’.

Numba aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo, aliichezea Zanaco kabla ya kutimkia Kankola Blades mwaka 2001.

Akiwa Kankola ambayo pia ni ya Zambia, alipata bahati ya kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Chipolopolo’ kilichocheza fainali za Afcon za mwaka 2000 na za miaka minne baadaye.

Mfumo wao wa uchezaji

Numba ni muumini wa soka la kutumia nguvu. Ameifanya Zanaco kuwa timu yenye kushambulia kwa kasi, nguvu na umiliki mzuri wa mpira.

Mfumo ambao unaonekana kuing’arisha Zanaco ya Numba kwa sasa ni 4-3-3 na 4-2-3-1. Ukiwauliza APR kilichowakuta kwa mfumo huu watakuwa na majibu mazuri.

Silaha yao ni kiungo, ushambuliaji

Siri kubwa ya Zanaco kufanya vizuri hasa dhidi ya APR, ni ubora wa safu yao ya kiungo na ushambuliaji. Katika eneo la katikati ya uwanja, Attram Kwame raia wa Ghana, amekuwa akifanya kazi yake kwa ufasaha akishirikiana na kiungo mkabaji, Siame Musonda.

Katika ushambuliaji, wanaye mkali Fashion Junior Sankala ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Urusi alikokwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa.

Junior mwenye umri wa miaka 21, anashirikiana na kaka yake Saith Sankala au Kennedy Musonda kuifanya safu ya ushambuliaji ya Zanacio kuwa hatari.

Hitimisho

Zanaco si wa kubeza hata kidogo, ni timu nzuri yenye ari na morali ya ushindi, hivyo basi, Yanga wanatakiwa kuwa makini na kucheza kwa tahadhari kubwa ikiwamo kupata ushindi mnono wakiwa hapa nyumbani.

Hiki ndicho kikosi cha Zanaco FC kinachotarajiwa kuwavaa Yanga kwenye mechi yao ya kwanza jijini Dar es Salaam.

Makipa: Racha Kola, Toaster Nsabata, Mangani Banda.

Walinzi: Ziyo Tembo, George Chilufya, Lee Ngoma, Taonga Bwembya, Chongo Chirwa, Peter Jacob Banda, Andrew Kwiliko.

Viungo: Richard Kasonde, Augustine Mulenga, Attram Kwame, Boyd Siame Musonda.

Washambuliaji: Fashion Junior Sakala, Saith Sakala, Kennedy Musonda, Ernest Mbewe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -