Friday, December 4, 2020

Zawadi maalum unayopaswa kumpatia unayempenda

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

KUMPATA anayekupenda si tiketi ya uhakika ya kupata furaha na amani katika mahusiano yako kama hujatimiza wajibu wako ipasavyo.

Furaha ya mahusiano inatengenezwa na namna wahusika wanavyotendeana. Unaweza kumpata mtu unayependana naye sana ila kama hamtendeani inavyotakiwa huenda baada ya muda mfupi uhusiano wenu ukafika tamati.

Ukiona mtu anakupenda sana usidhani hawezi kukuacha ama hawezi kutokukupenda baadaye. Tambua upendo huota mahali kwenye kujaliwa, kuthaminiwa na kusikilizwa.

Wanaopendana kwa muda mrefu, huwa na uwezo wa kuoneshana thamani zao katikamaisha.Katikamakalayaleo nataka nikujulishe zawadi ya uhakika unayoweza kumpa mpenzi wako na ikafanya uhusiano wenu kudumu na kuleta maana katika maisha yenu.

Zawadi ya uhakika kwa mapenzi wako ni kumuonesha unavyompenda na kuoekana kuijua na kuiheshimu thamani yake katika maisha yako.

Mpenzi wako ukimpa zawadi ya nguo atafurahi sana, ukimpa zawadi ya
simu atashukuru ila ukimpa zawadi ya kumuonesha yeye ni muhimu na wa thamani katika maisha yako utakuwa unajenga mizizi ya furaha ya kweli katika nafsi yake.

Hakuna kitu kizuri katika mapenzi kama kuhisi yule unayempenda naye anakupenda zaidi.

Kuna kitu watu wanashindwa kukitambua katika mahusiano yao.

Wengi waliopo katika mahusiano wanahaha usiku na mchana kutafuta njia ya kuonesha ni kwa kiwango gani wanawapenda wahusika.

Katika kufanikisha hayo, wengine kila siku wanawaambia wenzao kwamba wanawapenda ila wanahisi kama hawaamini.

Wengine wanajidhiki hata kununua zawadi za gharama kubwa kuonesha ni kwa kiwango gani wenzao wana umuhimu na thamani katika maisha yao.

Nataka uelewa hili. Zawadi kwa mpenzi wako ni kitu cha msingi. Kumwambia mwenzako namna unavyompenda inasisimua sana. Ila naomba utambue vitu hivi.

Zawadisikielelezopekeechaupendokwa mwenzako kwa sababu hata matapeli wenye pesa hutumia kama chambo kuwavuta wale wanaowataka na kuwatamani.

Pia kumwambia mwenzako namna unavyompenda inamfanya aelewe kidogo juu ya hisia zako kwa sababu binadamu huelewa zaidi kwa kuona ama kuhisi na sio kuambiwa.

Namna itakayomfanya mwenzako aelewe namna unavyompenda na kumuhitaji ni vile unavyoishi naye. Jiulize, namna unavyoishi naye kunapeleka ujumbe gani kwa mwenzako?

Mwenzako kupitia matendo na kauli zako anaiona vipi nafasi yake katika maisha yako? Nataka utambue kitu kimoja. Uzuri ama cheo chako si kigezo kikuu cha kumfanya aendelee kukupenda.

Utafanya akupende na akupe thamani stahiki kutokana na namna unavyomfanya ajione bora na wa thamani kupitia matendo na mtindo wako wa maisha.

Mwanamke anahitaji kuona thamani yake kwa mumewe. Aone anavyodekezwa, anavyosikilizwa na kutimiziwa hana na shida zake.

Anataka kupitia kauli na matendo ya mumewe ajiaminishe kuwa katika maisha ya mumewe, ye ni miongoni mwa binadamu bora na wenye thamani ya kipekee.

Halikadhalika kila mwanaume anataka kuona akiheshimiwa, kutiiwa na na kujaliwa na mke wake. Anataka kuhisi amri na makatazo yake kwa mkewe yatapewa thamani na heshima stahili.

Hakunamwanaumemwenyekutakamke wake alete ushindani na ubishani naye kila siku.

Mwanamke mshindani si ndoto ya mwanaume. Hata awe na sura na umbile zuri vipi. Hata awe na elimu na fundi kitandani kwa namna gani ila kwa tabia yake ya ushindani mwanaume wake atawahi kumkinahi na kuachana naye.

Mwanaume akiwa kwa mawanamke hupenda kuwa kama Simba mtawala. Hapendi kushindana na mwanamke wake na kama mwanamke atajifanya kichwa ngumu basi mwanaume husika atatumia maguvu na uwezo wake wote kuonesha yeye ni nani kwake.

Wanawake wengi wameharibu mahusiano yao kwa kudhani njia ya kumuweka sawa mume wake ni kupambana naye kwa mambo wanayotofautiana. Ni kosa kubwa.

Mwanaume hapendi kushindana na mwanamke. Mwanamke anapokosana na mwanaume bora atumie mbinu ya machozi ama kuonesha kaonewa.

Mbinu hii huwasaidia wanawake kwa sababu mwanamke makini hapendi kujiona anamuonea mwanamke hivyo mwanamke akiwa analia ama kutumia njia ya kuonesha kaonewa basi mwanaume husika huamua kuwa mpole na kumfanyia mwanamke jambo litakalo muweka sawa.

Kuza thamani yako kwa mwenzako kwa kumfanya ajione bora na akuone wa kipekee. Mahusiano ni taasisi inayohitaji umakini na hekima ili uweze kupata furaha na thamani ilipo ndani yake.

Bila umakini na ujanja stahili kila siku utakuwa unabadili wapenzi na kulalama jinsia fulani ni mbaya kumbe ubaya uko katika matendo na maamuzi yako.

Kila mmoja aliye katika mahusiano anahitaji kuoneshwa anapendwa, anajaliwa na kuthaminika. Bila vitu hivi mahusiano yako yatapoteza msisimko na hata kupelekea kutengana na mwenzako ingali ukiwa unampenda.

Instagram: g.masenga
Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia ( Psychoanalyst) ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -