Thursday, December 3, 2020

ZIJUE KANUNI ZA LIGI KANUNI YA 38: MWAMUZI ANAWAJIBU WA KUJIHESHIMU, NIDHAMU, MAADILI NA SHERIA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Na KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) lina jukumu la kusimamia mchezo wa mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha sheria na kanuni zinafuatwa.

Mchezo huu wa mpira wa miguu ambao unaongoza kwa kupendwa ikiwa ni pamoja na kuwa na mashabiki wengi duniani unachezeshwa kwa kufuata sheria 17 ambazo zimetungwa ili kuwa muhimili.

Sambamba na sheria lakini pia mchezo huo unaongozwa kwa kufuata kanuni za mashindano husika ambazo hutumika kutoa maamuzi iwapo mchezaji, kiongozi, mwamuzi ikiwa ni pamoja na mashabiki wanapokuwa wamefanya vitendo ambavyo ni kinyume na mchezo huo wa mpira.

Tunaposema sheria za mpra wa miguu na kanuni za mashindano ni vitu viwili tofauti lakini pia vinaweza kufanana katika maamuzi ambayo huweza kutolewa kulingana na kosa lililofanyika.

Sheria ni kitu ambacho kikishawekwa hakiwezo kubadilika labda kwa kufuata taratibu lakini kanuni zinaweza kubadilika muda na wakati wowote baada ya wahusika kukubaliana.

Wakati wa mchezo unapoendelea uwanjani au hata kabla ya kuanza kwa mchezo, matukio ni mengi hujitokeza huweza kutolewa maamuzi kwa kutumia sheria na mengine kanuni pale itakapobidi au vyote kwa pamoja.

Hivi karibuni katika mchezo uliozikutanisha timu za Yanga na Ruvu Shooting, mwamuzi Hamd Simba alimyima bao mchezaji Obrey Chirwa na baadaye alimpa kadi njano ya pili na kusababisha utata miongoni mwa mashabiki.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucus alisema kuwa baada ya kumtaka mwamuzi huyo kujieleza alidai kuwa hakuliona tukio vizuri na kwamba alichoona ni mchezaji kufunga goli kwa mkono na ndio maana alitoa maamuzi hayo aliyoyatoa.

Kulingana na maelezo hayo, Bodi ya Ligi baada ya kujiridhisha na ushaidi wa luninga, kwa kutumia kanuni za ligi kanuni namba 38 inayozungumzia Udhibiti kwa Waamuzi, kipengele cha 1(a) kwamba mwamuzi akishindwa kumudu mchezo kwa uzumbe, makusudi, woga, kutozingatia sheria na kusababisha kutokea vurugu mchezoni, kuhatarisha amani au kutia aibu fani ya uamuzi ikiwa ni pamoja na kushusha hadhi ya uamuzi ililazimika kumuondoa katika orodha ya waamuzi wa ligi kuu kwa msimu huu ikiwa ni pamoja na kufuta kadi moja ya njano aliyopewa awali mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi, kanuni namba 38 inasema mwamuzi na mwamuzi msaidizi atakayeteuliwa na kupangwa kuchezesha Ligi Kuu watawajibika kujiheshimu na kuzingatia nidhamu, maadili na sheria katika utekelezaji wa majukumu yake katika kiwango bora na kisichotia shaka.

Pia waamuzi hao wanawajibika kuwa na haiba na mwenendo bora wa tabia katika ushirikiano wake na wadau wengine wa mpira wa miguu.

Katika kipengele cha kwanza cha kanuni ya 38 kinasema kuwa mwamuzi atakayethibitika au kubainika kwenda kinyume na sheria au taratibu za mchezo wa mpira wa miguu atapata adhabu ya kufungiwa kati ya miezi tatu na miaka mitatu, kushushwa daraja la uamuzi, kuondolewa au kufutwa kabisa katika orodha ya waamuzi wanaotambuliwa na TFF ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa leseni ya uamuzi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -