Wednesday, October 28, 2020

MWISHO WA ROONEY MANCHESTER UNITED WAKARIBIA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

HALI halisi iliyopo kwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, ni kwamba mwisho wa maisha yake ndani ya klabu hiyo tayari umejulikana wazi.

Shughuli inazidi kuwa ngumu kwake kutokana na uwepo wa kiungo mbunifu kutoka Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan aliyesajiliwa katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

Raia huyo wa Armenia anasubiri kwa hamu jukumu la kucheza namba 10.

Na kwa namna anavyojituma mazoezini, Baba Kai yupo mbioni kuuachia usukani kwa nyota huyo raia wa Armenia na nyota wengine wanaoisubiri nafasi hiyo ndani ya United.

Huku Mkhitaryan akiendelea kusubiri, bado Mhispania Juan Mata na mchezaji ghali duniani kwa sasa, Paul Pogba wanavutana sharubu mmoja wao akitaka kujihakikishia nafasi hiyo ni ya kwake. Hii vita ni kubwa mno kwa Rooney.

Kocha wake, Jose Mourinho aliumiza kichwa majira yaliyopita ya kiangazi iwapo Rooney angeweza kuingia kwenye mipango yake.

Ukweli ni kwamba, asingeweza kumweleza moja kwa moja aondoke kwani kwa inavyoonekana ni kwamba Mreno huyo anataka kuona na anataka mashabiki wa Man United kumuona Rooney bado anaweza kufanya makubwa.

Wapo mashabiki ambao bado wanamkubali Rooney pale jijini Manchester na kuna wale wa kwenye mitandao ya kijamii ambao wanaonekana kuwa na mitazamo tofauti juu ya maisha ya nahodha wao aliyeifanyia timu hiyo makubwa kwa miaka aliyoichezea.

Tangu acheze chini ya kiwango dhidi ya Watford kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliomalizika kwa United kuchapwa mabao 3-1, Rooney hajapata nafasi kamili ya kucheza na jibu la swali la kwanini haanzi ni kwamba ameshaisha kiwango.

Amefanya mengi sana na mwili wake unagoma kutoa ile burudani tena huku akili ikitaka kwa nguvu.

Ile kasi aliyokuwa nayo iliyomfanya afunge mabao 34 kwa misimu miwili (2009-10 na 2011-12) haipo tena.

Zile pasi ndefu sasa hivi haziwafikii walengwa. Mashuti makali yamepungua.

Ilikuwa aondoke wakati Sir Alex Ferguson akimalizia muda wake ndani ya United lakini kocha aliyerithi mikoba, David Moyes, alimtaka aongeze mkataba na akaongeza lakini bado minong’ono ilikuwepo kwamba alishaisha kiwango.

Si ndani ya klabu pekee, hata timu ya taifa ya England ameshapoteza nafasi yake.

Mashabiki wameshamchoka na inakumbukwa kuwa alizomewa kwenye mtanange wa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia Urusi 2018 dhidi ya Malta.

Kwa miaka yote 15 ya kusakata soka la ngazi ya juu, huu ndio muda sahihi kwa Rooney kupumzisha akili yake na miguu pia.

Rekodi zake zitakumbukwa tu hata akiwa nje ya uwanja. Ndani ya United ana vita ya namba dhidi ya vijana wadogo kama Paul Pogba, Henrikh Mkhitaryan, Jesse Lingard, Marcus Rashford, Juan Mata na Anthony Martial.

Kuna nafasi ipi itakayomfaa Rooney? Hakuna.

Ukienda timu ya taifa ya England ana kazi kubwa ya kufanya ili kutetea nafasi yake na akiwa kama nahodha.

Anatetea nafasi yake dhidi ya nani na ni wachezaji wa aina gani kwa soka la sasa?

Kuna Jamie Vardy, mshambuliaji bora wa Leicester City msimu uliopita, mfungaji bora na aliyeisaidia timu hiyo kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kuna Dele Alli, kiungo mshambuliaji mahiri wa Tottenham Hotspur sambamba na mshambuliaji Harry Kane na mwisho kabisa kuna Daniel Sturridge ambaye anawania namba na washambuliaji wengine mahiri pale Liverpool kwa sasa.

Rooney ana nafasi gani katika pande zote hizo mbili?

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -