Friday, October 23, 2020

ZIMBABWE YA MAJANGA ITAVUNA NINI AFCON 2017?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

HARARE, Zimbabwe

ZIMBABWE ni miongoni mwa mataifa yatakayoshiriki Fainali za Afrika za mwaka huu (Afcon 2017).

Timu hiyo pia inafahamika kwa jina la ‘The Warriors’ na hii ni mara yake ya tatu kucheza mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Itakumbukwa kuwa Zimbabwe ilishindwa kushiriki michuano hiyo mwaka 2004 na mwaka 2006.

Katika fainali za mwaka huu zitakazofanyika nchini Gabon, Zimbabwe itamtegemea staa wao anayekipiga katika klabu ya KV Oostende ya Ligi Kuu nchini Ubelgiji, Knowledge Musona.

Musona ndiye anayeongoza kwenye orodha ya wapachikaji mabao klabuni hapo.

Lakini pia, jicho la mashabiki wa Zimbabwe litakuwa kwa nyota wao, Khama Billiat, anayetamba na Mamelodi Sundowns ya Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.

Mastaa wengine wanaotarajiwa kuibeba Zimbabwe ni pamoja na beki wa AC Sparta Praha ya Jamhuri ya Czech, Costa Nhamoinesu.

Mpachikaji mabao hatari wa Helsingborgs IF ya Sweden, Matthew Rusike na Tinotenda Kadewere  wa klabu ya Djurgardens IF.

Zimbabwe imeingia kwenye michuano hiyo ya Afcon ikiwa inashika nafasi ya 102 kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa Ulimwenguni (Fifa).

Ukiachana na viwango hivyo vya Fifam, timu hiyo inakamata nafasi ya 29 kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf).

Katika mechi za kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo za Gabon, Zimbabwe ilishinda mechi zake nne kati ya sita.

Hata hivyo, imesemekana kuwa tatizo la uchumi linaweza kukiangusha kikosi hicho na hatimaye kushindwa kufanya vizuri nchini Gabon.

Imeelezwa kuwa Chama cha Soka nchini humo (ZFA), kinakabiliwa na madeni na mara kadhaa kimeshindwa kulipa mishahara ya wachezaji na wafanyakazi wengine wa benchi la ufundi.

Taarifa zilizopo ni kwamba, ZFA wamekuwa wakitembeza bakuli kukamilisha baadhi ya mambo yanayohusiana na mchezo wa soka ikiwamo kuwalipa makocha.

Mbali na hilo, kudorora kwa uchumi nchini humo kumesababisha hata kupungua kwa idadi ya mashabiki wanaohudhuria viwanjani.

Ikumbukwe kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Zimbabwe iliondoshwa kwenye mchakato wa awali wa kufukuzia tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika Urusi.

Zimbabwe walikumbana na adhabu hiyo kutoka Fifa baada ya kushindwa kumlipa kocha wao, Jose Claudinei Georgini, mshahara wa Dola za Marekani 67 000.

Sambamba na majanga hayo, timu hiyo itakuwa Kundi B katika mashindano ya Afcon 2017 ambapo itakuwa na kibarua dhidi ya Senegal, Algeria na Tunisia.

Senegal ndio wanaokamata nafasi ya kwanza kwa ubora wa soka barani Afrika, Tunisia wako nafasi ya tatu, huku Algeria wakiwa nafasi ya tano.

Kwa maana hiyo, Zimbabwe wana kibarua kizito cha kuvuka hatua ya makundi nchini Gabon. Lakini si rahisi kuiponda kabisa Zimbabwe na hata mchambuzi mkongwe wa soka nchini humo, Stanley Katsande, anaamini hivyo.

“Zimbabwe walikuwa moto wa kuotea mbali wakati wa mechi za kuwania kufuzu (Afcon 2017),” alisema Katsande alipokuwa akihojiwa na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP.

“Huenda wakashindwa kuwa kinara wa kundi lao lakini vijana watashangaza kwenye michuano hiyo licha ya kudharauliwa.

“Wakati wengi wakiamini kuwa watakuwa vibonde kwenye kundi lao,  naamini watafanya kitu. Watakutana na timu bora barani Afrika na wanatakiwa kutulia kwa asilimia 110.”

Naye mhariri wa gazeti la Daily News, Nigel Matongorere, alimtaka kocha wa kikosi hicho, Callisto Pasuwa, kuzichakaza timu zinazotajwa kuwa kubwa Afrika akiamini zina mapungufu makubwa kwa sasa.

“Katika michuano miwili iliyopita ambayo Zimbabwe ilishiriki, ilishindwa kutinga hatua ya robo fainali,” alisema Matongorere.

“Safari hii, Pasuwa ana wachezaji na bahati, Warriors wanaweza kufanya maajabu.”

Zimbabwe ina historia nzuri kwenye soka la Afrika hasa kwenye miaka ya 1990 ambapo kikosi hicho kilicheza mechi 13 bila kufungwa.

Kwa wafuatiliaji wa soka, watakumbuka kuwa kipindi hicho, timu hiyo ilikuwa ikinolewa na kocha raia wa Ujerumani, Reinhard Fabisch.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -