Friday, December 4, 2020

ZUENA BINT MSASAMBUKO (11)

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ILIPOISHIA JUMANNE…

‘Faridaaa!’ Mama akaita akimchoma kwa vidole vyake mapajani

‘Eeh mama wanaume hawashikiki hawa bila dawa….watu kibao wanahangaika  hivi  hivi ndoa hakuna tutazaliana hapa kama panya’ Farida kajitetea akiungwa mkono na shangazi…SASA ENDELEA..

‘mama yenu kazubaa, ungechangamka wifi wanao wote wa kike wangekuwa kwa waume zao…..watu tulicheza makaburini uchi mpaka mwanangu Zawadi akaolewa…..safari ya pili tulipasua nazi saba njia panda saba….tukachimbia vya kuchimbia na unyayo tukamchota wiki hii….’ Shangazi akatuonyesha kidole chake cha shahada akiendelea kusema….’…Moja!!, mbona walikuja wamebebana kama zabibu kuja kutoa mahari Samia akaolewa, sitaki mchezo wa mtu kumtia mwanangu mimba halafu amuache aniozee ndani kama ndizi mbivu….mitishamba tu kwisha kazi mengine mbele kwa mbele!’

‘Mama unayasikia hayo’ Farida akashabikia

‘Lakini shangazi mi siyaamini haya ya waganga sana kwanini usiwe na mtu anayekupenda toka moyoni nawe ukajua hili pendo halali si la mitishamba?’ Subira akalalamika.

‘Hilo pendo la kweli Subira liko wapi?….umeishi na yule fundi cherehani mwaka sasa hata mahari hajaleta, lile ndio pendo halali?’ shangazi akamdaka Subira

‘Kwa sasa hana ila akipata ataleta tu!’ akajitetea Subira

‘Nyooo! Ataleta tu…wanaume unawajua, unawasikia au unawasoma tu kama riwaya?…. atakata kuni na wewe na moto mtawasha wote ila wakati wa kuota huo moto atauota na yuleee si wewe mliyekata kuni naye, wanaume wana hila ya muwa kujaa mafundo….changamkaaa!’ shangazi akanesanesa akishindilia maelezo yake.

Tukatazamana na Subira, mama ndio kabisa alikuwa akitabasamu na kutikisa kichwa. Hakuamini katika hayo mambo ila ndio Farida na shangazi walishamzidi nguvu.

‘Kama kweli unamtaka sema nikupeleke kwa mzee mmoja anaitwa Singangala yuko hapo Kongowe ….dawa zake ukioga na kujifusha  siku saba mambo kwenye mstari ukijumlisha masharti yake hata kama alikuwa anataka kuoa na mahari kashaitoa, ataacha vyote akurudie mbio chini ya miguu….Singangala huyo! Super mkomesho!’ akanadi shangazi mie moyo ukiwa mzito kwelikweli

‘Ngoja nikusanye vijisenti shangazi unipeleke uko, kuna mtu anataka arudi kuniosha miguu kwa machozi yake’ Farida akadakia na kutufanya tucheke tena. Maongezi yakawa maongezi. Sikuafiki wakati ule nikamwambia shangazi anipe muda nikae sawa.

Usiku ule mama akanijia chumbani nilikokuwa nikilala na watoto wa dada zangu, huku mama akilala na Farida na mtoto mdogo wa Farida. Baada ya kuhakikisha amewafunika wajukuu zake vizuri akanifuata pale kitandani. Tukazungumza hili na lile akiomba na pesa kidogo akanunue nguo za kuvaa maulidi ya mjukuu wake. Nikamwahidi wiki iliyofuata ningempatia, mama akashukuru na akinibariki na dua zake. Akakumbuka!

‘Mh mwanangu! Aliyoyasema mama Hijja!….hapana mi mapenzi ya kusukana akili na kufanyana mazezeta siyapendi na siyaamini. Kama Salehe anakupenda na imeandikwa awe wako atakuja tu hata ipite miaka mingapi, hata aoe wangapi kama anakupenda atarejea tu Mwenyezi Mungu atawaleta tu pamoja, tofauti na hapo mwanangu utageuka mchawi uchokoze hasira za Mtume bure…. Lakini vipi kuhusu Madobe?….kijana wa watu ametoka na wewe mbali sana, naona unajisahau na unasahau fadhila zake’ mama kaongea kwa upole akiirudisha akili yangu kwa Madobe.

‘Usiache mtu akuamulie maisha yako ya kimapenzi ili lolote likitokea hutomlaumu mtu!…nitazame mimi mama yako…niliolewa na Tupajembe kwa kumpenda mwenyewe na nikijua naenda kuwa mke wa pili…yananikuta machungu, yananikuta maumivu ila sijuti kwa vile niliamua nikiwa timamu kichwani….’ Mama akaongea kwa hatua akinipigapiga begani katika namna ya kunifariji.

‘…na hivi unavyosusuika na huyo Suriama umkumbuke Madobe amekutunza tangu ungali mtoto, katika shida zako zote Madobe amesimama na wewe, niliugua kipindi kile nusu ya kufa, Madobe alijitoa kwa hali na mali kama mwanangu wa kumzaa kunitafutia mitishamba, kakusaidia mengi sana leo hii unataka kutupa jamvi kwa mkeka wa kuazima?…atajisikiaje kijana wa watu Zuena?….au ni kwa vile Salehe ana pesa?….mmh! Sijui ila nakukumbusha tu kuwa pesa maua mwanangu Mungu anaweza kumshusha akampandisha Madobe sijui utamkimbilia tena mtoto wa watu?…..kaa chini uamue moja! Usije ukaruka dimbwi la maji ukajikuta kwenye bahari ya tope!’ Akamaliza hotuba yake, akiniachia mawazo lukuki. Usingizi haukuja kwa wakati ule nilikuwa nikiwaza na kuwazua.

Moyo ulishindwa kuamua nimpende nani, moyo ulishindwa kutulia ukamchagua fulani. Madobe! Nikahisi huruma ikiniingia, nikatulia kwa muda msukumo mwingine wa kutaka kumuendea Salehe kwa mganga ukinijia. Mbona  kila mtu anafanya uganga, kwani mimi nitakuwa wa kwanza? Nusu saa nikahisi nikibadili mawazo. Nitulie tu na Madobe! Ila moyo nao ukawa kigeugeu mara wamtaka tena Salehe! Nikahisi kugeuka kichaa muda si mrefu. Nikajituliza na mawazo yakanipa usingizi ikiwa imeshatimu saa 8 usiku!

*********

Siku mbili mbele, mama alizidi kunisisitizia nitulie kwanza kabla ya kuamua kwenda kwa huyo mtaalamu. Nikawaza na kuwazua ukichanganya na ushauri wa Subira nikaona Salehe alikuwa ananipotezea muda tu. Tulikuwa watu wawili tofauti toka dunia tofauti, tulikuwa kama lila na fila. Havichangamani!

Siku chache kabla ya Maulidi ya Rahim, mtoto wa kaka Shabani, baba alikuja pale nyumbani, akaonana na mama na kuzungumza kuhusu hiyo sherehe. Baba akalibeba jukumu la kuongea na Shabani ambaye alikubali kufanyia pale nyumbani. Wiki hiyo ya maandalizi angalau palisafishwa na kukarabatiwa hapa na pale.

Jumapili hii kabla ya maulidi, Madobe akaja nyumbani, akimletea mama nguo pamoja na mimi. Akanitoa na kunipeleka Kariakoo kununua viatu na vitu nilivyohitaji. Sikuwa na makuu ya kuhitaji mamilioni. Nilikijua kipato cha Madobe na juhudi zake hivyo nilikuwa na adabu katika kufanya manunuzi ya vitu vyangu. Nikatoka uko na furushi la vitu, mwenyewe Madobe akinipitisha saluni kutengeneza nywele zangu. Alinijali!

Siku tatu mbele akaleta mchele kilo kadhaa kwa ajili ya maulidi. Mungu anipe nini, kati ya watoto wa mama  na mimi nilionekana kuwa na mwanamume wa maana ukiachilia mbali Farida ambaye kwa wakati huo alikuwa na mwanamume aliyekuwa ana iliki mashine ya kusaga mahindi hapo hapo Kibaha.

Tatizo alikuwa mume wa mtu hivyo alikwenda naye kwa kujificha ficha. Huyu shemeji alifanya tukavaa dhahabu siku hiyo japo vikuku na kupata hela ya mashauzi ya kumtunza mtoto wa kaka.  Kilichokuja kuwaachanisha ni kitendo cha Farida kumtukana mke wa yule mwanamume akilazimisha kutambulika kama mke mwenza. Mapenzi ya kafia hapo na huduma zikaishia hapo!

Siku ya maulidi tulifunga mtaa, mama zangu wa kambo waliingia na coaster likipeperusha khanga iliyoandikwa ‘ Nafanya mambo kwa raha zangu sifanyi fahari kama wenzangu’. Nakubali maana nzima ya maulidi ilipotoshwa ikatawaliwa na hekaheka za mashauzi na maonesho. Tukawapokea na kikundi cha ngoma maarufu hapo kibaha na wimbo wao ‘mtoto majaaliwa’ tulilizunguka coaster kwa mbwembwe uku tukiimba sambamba na kile kikundi. Tulipania haswa hii shughuli ifunge mtaa.

Tulijimwaga kwanza tukiimba na kucheza kwa mtindo wa kunema kama mwali. Wazaramo utusikie tu ukichanganya na ukweli kuwa mama zangu wa kambo walikuwa wakwere, basi shughuli ilipata washughulikaji shughulini. Na kwa jinsi tulivyokuwa tukinema kwa ustadi tuliwavuta hata wale waliojitia uzungu na kung’ang’ania mkekani. Walitoka wenyewe ndani wakajiachia pale nje. Narudia tuliufunga mtaa!

 

Baada ya hekaheka ya mapokezi tulisaidiana kushusha mikungu ya ndizi na baadhi ya vyakula, tukavipeleka uani, uko kulikuwa na kundi la wanawake wa mtaani wakingojea kuanza upishi. Shughuli zikapamba moto na kwa vile tulikuwa wengi na wapangaji walijitolea majiko yao saa saba mchana shughuli ya kupika ilikuwa imeisha. Na punde tukasikia hekaheka nje Nursati alikuwa anaingia na mwanae Rahim bin Shabani Msasambuko.

Tuliweka chuki kando tukamlaki kwa bashasha zote tukimpokea mjukuu wetu, mwanetu! Shughuli ya kusoma dua iliongozwa na Ustaadh Pangamoja wa msikiti mkubwa hapo Kibaha pamoja na mwenziwe Maalim Jumar. Baada ya kukamilisha kila kitu, wanawake tulikuwa na upande wetu wanaume na upande wao. Suala la maakuli likafuatia, sisi mnaotuita waswahili Mungu katupa mkono wa kupika. Usiombe kuhudhuria shughuli ya waswahili ukaalikwa kula, utasahau njia  iliyokuleta!

Kasheshe ikaanzia hapa! Wakati watu wakipata chakula nilitoka nje na kusimama nikiegemea moja ya magari yaliyokuwa yamepaki hapo nje. Nikawa naongea na simu ya yule boss wangu wa posta. Hakuweza kufika ila alitaka kunipa hongera na salamu za mama.

Nikiwa nimesimama hapo Madobe alinifuata na kusimama kando yangu akingoja nimalizane na simu yangu. Kibagarashia chake cheupe na ile kanzu yake nyeupe ilimfanya nimuone kama mfalme! Alisimama hapo akinirekebishia pini kwenye mtandio wangu kichwani. Ghafla Salehe akatokea upande huo huo tuliokuwa tumesimama akiwa ameongoza na Kianga. Wakanipita wakitutupia Asalam aleykum. Tukaitikia!

 

Itaendelea kesho

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -