Thursday, December 3, 2020

ZUENA BINT MSASAMBUKO (12)

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ILIPOISHIA JANA….. Alisimama hapo akinirekebishia pini kwenye mtandio wangu kichwani. Ghafla Salehe akatokea upande huo huo tuliokuwa tumesimama akiwa ameongozwa na Kianga. Wakanipita wakitutupia Asalam Aleykum. Tukaitikia!

SASA ENDELEA…..

Nilishusha pumzi ila sikubabaika, nilishaanza kuukubali ukweli kuwa hatuwezani. Nikamalizana na simu na kumgeukia Madobe

‘Haya vipi baba?’ nikamuuliza

‘kuna kitu nataka tuongee kabla sijaondoka hapa’ akaanza maelezo akinitazama kwa upole. Nikayakuza macho yangu, nikiikusanya mikono yangu na kuipishanisha kifuani hali nikijiegemeza vizuri kwenye lile gari

‘Nina ugonjwa wa mchecheto, bora tu unambie sasa hivi hiyo baadae unaweza kusahau nikalala tumbo likinisokota…niambie tu’ nikamuasa nikielewa sababu za yeye kuniambia muda ule ni kuogopa kusahau.

‘Nimenunua kiwanja Boko, si kikubwa ila nimeandikisha jina lako kama zawadi ya mapenzi yangu kwako, nilitaka wikendi ijayo twende ukione’ akaongea taratibu kama kawaida yake. Nikamtolea macho zaidi nikicheka kwa sauti na kutamani kumkumbatia ila mazingira hayakuniruhusu. Moyo mweupe nikayaona mapenzi ya dhati ya mwanaume huyu aliyenitazama kama mkewe tayari.

‘Asante!’ Nikamjibu nikiuma midomo yangu na kuzuia ile hali ya kutaka kucheka tena maana moyo wangu ulijaa furaha mno namaanisha kupitiliza. Tukaongea hili na lile tukarudi ndani ambako watu walishamaliza kula kuanza kuburudika na kumtuza mtoto ikiwemo kupiga picha.

Nikapita pembezoni mwa nyumba nikiwahi ndani kumng’ata sikio mama na Subira kuhusu zile habari njema. Kabla hata sijaimaliza ile kordo nikamsikia Kianga akiniita kwa sauti. Nikageuka haraka na kumtazama, alikuwa na Salehe. Nikawapungia mkono na kumalizia safari yangu.

Kwanza niseme ukweli, gauni nililovaa siku hiyo lilinikaa vyema, pili nywele zangu kichwani zilifanya uzuri wangu uchomoze maradufu, tatu nilikuwa nimepambwa haswa na mama yangu mzazi, hivyo sikuona ajabu vijana kwa wazee kunitumbulia macho. Ilikuwa haki yao!

Jioni giza lilipoanza kuingia watu walianza kuondoka, wakabaki watu wa mtaani walioamua kuweka muziki na kuburudika. Nami nikatoka kuwasindikiza baadhi ya marafiki zangu. Wakati nikirejea na Subira, Kianga akanijia mbio nyuma

‘Zuena, Salehe anakuita’ akanieleza uku akihema

‘Anamuitia nini?…hebu twende bwana’ Subira akanivuta mkono, nikang’atua mkono wangu na kumgeukia kianga

‘Ananiitia nini?’

‘Mi kijumbe tu, sijui anachokuitia’

‘Yuko wapi?’ nikazidi kuhoji nikimtia Subira hasira kupitiliza

‘Yuko pale’ akanionyesha kwa kidole eneo la njia panda ya kuelekea kwao. Nikaguna na kumtazama Subira aliyekuwa amenikunjia ndita kama matuta. Shetani wa mguu mmoja akanivaa nikachanganya miguu nikimwacha Subira ananiita kwa sauti ya kukereka, kichwani nikipanga kumfikia na kumwambia asinizoee.

Nikamfuata Salehe pale alipokuwa amesimama. Akanilaki na tabasamu lake murua. Akinitazama kwa bashasha.

‘Umependeza sana leo’ akanisifia, mwenyewe jeuri zikianza kuporomoka. Sikujibu!

Akanikaribia zaidi, uzuri tulikuwa eneo lisilo na mwanga, akanisogelea zaidi mkono wake wa kushoto ukikizunguka kiuno changu na kunibana sawia kifuani pake. Akauvuruga mfumo wa fahamu zangu haraka kuliko kawaida. Nikahisi zile pumzi za ajabu zikinijaa kifuani, mwili ukitetemeka. Akanibusu mdomoni, kwisha habari yangu!

Nikadondosha simu iliyokuwa mkononi mwangu na kupenyeza mikono yangu kati kati ya mbavu zake na kuukumbatia mgongo wake kwa bidii, nikilikubali busu lile toka moyoni, nikilegea na kuruhusu mkono wake wa kulia ulikamate titi langu sawasawa na kuliminya. Nikagugumia utamu! Nikasahau shida zote za duniani humu kwa sekunde tu nikawa kama naikaribia pepo!

Ghafla nikasikia sauti!

‘Kheeee! we Malaya vipi!’ akaita huyu mtu, tusi lile likitosha kuziondoa zile hisia zote na  kunirejeshea nguzu zangu. Sauti ya kike!

Nikajitoa maungoni mwa Salehe na kugeuka! Alikuwa Raya Khalfani. Nikiwa bado nimemtumbulia macho huku midomo ikiwa inamwemweseka mwanamke yule alinivaa kwa ghadhabu.

Salehe akijaribu kuwahi kusimama kati yetu na akachelewa alishanikamata na kunivutia kwake. Alinikung’uta ngumi utasema alivaa mawe mkononi.  Salehe akatusogelea akijaribu kutuzuia na kumkanya Raya aache ugomvi. Hawakusikilizana! Nayajua yote lakini si kupigana wallah!

Salehe alijaribu kutuachanisha kwa nguvu zote ila huyu mwanamke alikuwa na nguvu utadhani alininywea  uji wa saruji kabla ya hapa. Yote kwa yote alinikong’ota si mchezo! Mpaka nakuja kunasuliwa mikononi mwake nilikuwanyang’a nyang’a sitambuliki kisogo kiko wapi wala uso uko wapi. Nilipigwa hasa!

Sidhani kama nilimwachia maumivu yoyote zaidi ya yale aliyopata baada ya Farida na Mwanahija kusikia nilikuwa napigwa mtaa wa pili hapo wakavamia kama jeshi, dakika mbili tu alikuwa chini amenyoosha mikono juu akiomba aachiwe. Mwanahija alimtandika kwelikweli mpaka Mzee Masoud alipotoka nje na kuamuru ugomvi uishe. Salehe alikuwa ameumizwa begani wakati akiamulia.

Nikatoka pale nikikokotwa kwenda nyumbani…nikamkuta Madobe nje! Hakunisemesha alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha akanipita na kuingia katika gari alilopata lifti, asinipe hata pole wala kunisemesha chochote. Nikaumia! kweli yamenikuta!…. Nikamchukia Salehe sasa, nikamchukia kabisa, sikutaka hata kumuona tena. Mama nusura akeshe akinigombeza na kunibeza! Nikalia jamani, nikaumizwa zaidi na aibu iliyonikuta. Mtaa wangu naujua mimi!  Nilijua usiku wa siku hiyo nilijadiliwa vitandani kama sala ya kulalia.

Usiku wa siku hiyo Salehe akanitumia ujumbe katika simu

‘Zuena, pole mpenzi, hata mimi sijapenda kilichotokea na wala sikujua kama huyu binti angekufanyia hivi. Niwie radhi mama. Nakupenda na nataka ujue sijaanza leo kukupenda na sijui kama nitakuja kuacha kukupenda. Nikaurudia ujumbe ule mara tatu. Nikaitupa simu kule, SIKUTAKA KUMUONA TENA, NILIMCHUKIA GHAFLA.

Jua la asubuhi ya siku hii lilikuwa kali kupitiliza, saa mbili na nusu jua lilikuwa linachoma mithili ya jua la saa saba. Ndio kwanza nilikuwa nimeamka na ukizingatia nilikuwa nina mapumziko ya siku mbili baada ya kuripoti kwa boss kuwa naumwa, sikuona haja ya kuamka alfajiri na maumivu yale niliyokuwa nayo.

Kipigo cha jana kiliniingia hasa, nilikuwa nimevimba sehemu mbalimbali za mwili wangu na kupata mikwaruzo shingoni na  pamoja na kuumia pembezoni mwa mdomo. Jicho langu la kulia lilikuwa limevimba kwa juu na kufanya weusi wa kuvilia damu, mgongo ulikuwa unauma kutokana na kutandikwa ngumi za mgongo achilia mbali alama ya kung’atwa begani niliyokuwa nayo. Niseme tu nilikuwa na maumivu karibia mwili mzima.

Nilinyanyuka toka pale kitandani na kulifunga vizuri pazia lililokuwa limefunguliwa nusu, mwanga wa jua uliokuwa ukiingia kupitia dirishani ndio hasa ulionitoa usingizini. Nikapiga miayo huku nikikitazama chumba namna kilivyokuwa ovyo. Matandiko wanayotumia kulalia watoto yalikuwa palepale. Nikakitandika kitanda changu na kuiendea meza ndogo iliyokuwa ikitumika kuwekea vipodozi, nikachukua mswaki na kuuwekea dawa.

Nikaliendea taulo lililokuwa juu  ya kamba chumbani hapo, nikalitupia begani nikipita kwa kuyakanyaga yale matandiko na kutoka nje,  sebuleni hakukuwa na mtu zaidi ya mtoto wa Farida mdogo aliyekuwa amelala kwenye kochi, vikombe vya chai na punje za wali zilikuwa zimetapakaa kila kona, nikasonya nikikereka na ile hali ya uchafu. Nikaelekea uwani na kumkuta mama akimsuka Farida, shangazi alikuwa akinywa chai na vitumbua kando yao huku Mwanahija akikata kabichi juu ya sinia lake alilokuwa amelipakata mapajani.

Nikawasabahi na kuliendea dumu la lita 50 lililokuwa na maji na kulikalia. Shangazi akaharakia kumeza kitumbua chake na kunigeukia

‘Umeyasikia ya leo?’ Akaanza na swali mwenyewe asijue ni kiasi gani sikuhitaji kusikia lolote kwa wakati ule. Nikaugeukia mlango ule wa uani unaoshika korido ndefu kuelekea mpaka nje barazani. Nikamuita Aisha, mtoto mkubwa wa Farida

‘We Aisha hebu njoo kwanza maana waitika tu kuja huji’ nikakaza sauti baada ya kumsikia akiitika bila kuja

‘Amefanya nini tena’ mama akaniuliza

‘Chumbani hakujatandikwa hapo sebuleni hata hapatamaniki’ nikalalamika nikimtazama Aisha anavyojongea pale uwani kwa mwendo wa kukimbia kimbia.

‘Kaondoe matandiko pale chumbani haraka kisha ufagie hapo sebuleni’ nikamtundikia kazi

‘Ma’ mdogo kila siku mimi ndio natandika mwambie na Mwanahamisi sasa’, akalalamika Aisha akimtaja mtoto mkubwa wa Mwanahija, akazungumza kwa kithembe kutokana na kukosa yale meno ya mbele. Tukamcheka shangazi akizidi kumtania na kufanya Aisha auvute mdomo mbele na kununa. Akachukua mfagio uliokuwa nyuma ya mlango na kuelekea ndani. Shangazi akarudia kauli yake ya mwanzo na kunifanya sasa nimsikilize bila kupenda.

‘Niyasikie wapi nami nilikuwa nimelala ndani’ nikamjibu.

‘Baba yake Raya kaenda polisi, kasema mwanae alivamiwa na wahuni na majambazi sugu sijui yanaitwa Mwanahija, Farida na Zuena na kupigwa na kuporwa mihela, midhahabu na migold… upo hapo?’ shangazi akanipa habari za kushtua lakini uwasilishaji wake ulifanya wote pale uwani tucheke.

 Itaendelea Kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -