Saturday, November 28, 2020

ZUENA BINT MSASAMBUKO (2)

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA LAURA PETTIE,

ILIPOISHIAN JANA…. sina kitu, nisaidie kama unazo’ akaongea kwa masikitiko kiasi cha kuhisi kumhurumia. Ile hasira nil iyokuwa nayo juu yake kwa kutokuja kama tulivyokubaliana ilianza kuyeyuka. Nikamuonea huruma.SASA ENDELEA..

 ‘Nitakutumia meseji baadaye nikujulishe kama ninazo na pia….’ Nikasikia mlio wa kukatika kwa simu. Nikacheka nikijua salio lilishamuishia. Nikarejea kitandani na kujitupa chali nikiitazama dari bila kuitambua akilini. Dakika mbili nzima nilitulia nikiwaza, nikipanga na kupangua.

Nikakigeuza kichwa changu na kuutazama mkoba wangu uliokuwa na hela. Laki!…mahitaji lukuki! Nikimpa 50 mie nitabaki na nini?…hapa ndani tutakula nini?. Baba yangu mzazi alikuwa Kibaha kwa Mathias kwa mkewe mdogo na ilikuwa imepita mwezi hajakanyaga pale nyumbani na hakujua tulikuwa  tunaishi vipi. Tulishamzoea awepo asiwepo yetu mamoja!

Nikatoka kitandani pale nikiliendea kapu lililokuwa nyuma ya mlango na kutafuta dera langu la hudhurungi na kulitupia mwilini, nikarudi kitandani na kuchukua sendozi zangu chini ya uvungu, nikaliendea dirisha na kujitazama kwenye kioo nilichokuwa nimekiegesha hapo dirishani na kujihakikishia nilikuwa sawa usoni. Nikatoka.

Miguu yangu iliniongoza kwenye vichochoro kadhaa nikaibukia mtaa wa pili, nilikuwa naelekea kwa rafiki yangu Subira. Pengine kumsimulia haya madhila yasoisha kungenipa ahueni. Alishanisikiliza sana pengine niseme kusikilizana maana tulikuwa tukipeana zamu kupokea vichapo vya shida!

Umasikini matusi! Uusikie kwa jirani ama uusome magazetini. Nikaishika njia iliyokuwa inapandisha kuelekea kwa Subira. Na mguu wangu wa heri nilimkuta akikanda unga wa maandazi uani. Ile kuniona akacheka, akacheka kwelikweli nusura agonge chupa ya cocacola iliyokuwa na mafuta ya kupikia

“Utasutwa Subira!….haya kinachokuvunja mbavu?” nikamdaka juu juu nikiiendea ndoo ya kufulia iliyokuwa umbali mfupi na kuipachika chini nikaikalia. Nikaondoa ushungi wangu na kutulia nikimngoja subira amalizie kicheko chake.

“Una maisha marefu Zuena kupita reli ya kati, muda huu…huu muda dada katoka Salehe hapa …muda huu huu nikijua pengine mmepishana hapo koridoni.”

‘Aka!…sijamuona mtu wala paka hapo koridoni,” nikakana nikibetusha mabega yangu. Moyo ukisusuika kulisikia jina la Salehe.

“Haya kaja kufanya nini?” nikauliza moyo ukizidi kunipaparika tumbo likinichefuka, nikitamani kuingia msalani muda huo. Subira akacheka, akacheka kicheko kirefu kilichoanza kunikera. Nikaufinyanga mtandio wangu na kumpiga nao.

“Hebu bwana wee….nambie basi Salehe kaja kufanya nini?” nikazidi kukereka zaidi baada ya Subira  kuacha kucheka na kunitazama kwa pozi. Midomo ikimwemweseka katika hali ya kujaribu kukizua kicheko chake. Akagongesha mikono yake hewani na kuitanua mithili ya mtu apokeaye dua.

“Salehe kaja hapa jioni hii kanambia anaoa,” akasema kwa tashtiti akikazia neno kuoa mara mbili mbili

“ANAOA!”nikamtupia swali mate yakinikauka mdomoni ghafla, mchafuko wa tumbo ukinizidia mara mbili, nikatunduwaa kwa sekunde kadhaa mwili ukishikwa na fadhaa. Nikahisi pumzi zilizotoka zikipishana uzito na zilizoingia, mwili ukasisimka. Nikamtumbulia macho Subira kana kwamba nilitaka ayarudie maneno yake lakini katika lugha ya kueleweka zaidi. Hakurudia na zaidi akacheka!

Shida nilizokuwa nikiwaza zikatawanyika na kukiacha kichwa changu kitupu mithili ya ukumbi wa dansi. Nikashusha pumzi kwa nguvu na kujilazimisha kuguna hali nikitafuta namna ya kuituliza nafsi yangu. Nikakosa!

Moyo ulishikwa na maumivu ya ghafla, sikuhimili uzito wa taarifa, mshipa wa uchungu ukanikarahisha kwa kuniletea machozi bila kuyatarajia. Nikapigana nayo kwa kila hali yasinitoke mbele ya Subira. Nikaweza!

Subira aliyekuwa anaendelea na kukanda ule unga akaachana ghafla na ile kazi na kunitazama tena. Safari hii akiwa kimya, alionekana kuisoma hali yangu pasipo kuipatia tafsiri kamili kama taarifa iliniumiza kwa kiwango gani.

“Anamuoa nani?” nikamuuliza Subira kwa sauti ya kitetemeshi. Akili yangu na moyo vikiwa haviko tayari kulikabilia jibu nitakalopata.

“Raya!” akanijibu kwa sauti kana kwamba alitaka kunisuta

“Raya?” nikalirudia jibu kwa mtindo wa swali, nikikosa balansi ya kukaa juu ya ile ndoo na taratibu nikaiacha na kukaa sakafuni. Nilichoka, niliduwaa zaidi nikaivuta pumzi na kuiteremsha huku nikisikilizia maumivu makali ndani ya moyo wangu. Nikaumia haswa!

Subira akajikusanya na kunyanyuka, akiondoa masufuria yake na vifaa vyake na kuvipeleka ndani. Akarejea na kuketi mbele yangu. Akinibwagia shungi langu mikononi.

Ikawa kama alinipa ruhusa ya kulia, ikanitoka kwikwi iliyoruhusu machozi yanitoke. Nikalia! Nikalia kwelikweli…

“Kulia hakusaidii kitu shost…hapa ni kujipanga tujue cha kufanya maana ndoa ni wiki ya tatu tangu leo, bado tuna muda wa kufanya kumrudisha Salehe,” Subira akanisemesha, akinipa moyo pengine na kuituliza akili yangu lakini wapi, kwa muda ule hata angeongea lugha za malaika nisingemwelewa.

Salehe Masoud, kijana jamali suriama mtanashati, weupe wake wa mchanganyiko ulinakshiwa vema na urefu wa kadiri ulijengwa katika mwili mzuri wa kiume ulioweza kumvutia mwanamke yeyote popote, uso wake muang’avu ulibebwa na tabasamu zuri liliweka bayana vishimo bashasha (dimpose) vilivyoweza kumwezesha bibi yeyote seuze binti kama mimi, kijana aliyefanikiwa kuuteka moyo wangu miaka miwili iliyopita akiwa mtoto wa Mzee Masoud Abdulatif na mkewe wa kiarabu, mzee mwekezaji aliyekuja Kibaha enzi hizo na kuwekeza katika sekta ya ujenzi.

Itaendelea kesho…

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -