Tuesday, November 24, 2020

ZUENA BINT MSASAMBUKO (3)

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

TABASAMU zuri liliweka bayana vishimo bashasha (dimpose) vilivyoweza kumuwewesesha msichana yeyote kama mimi, kijana aliyefanikiwa kuuteka moyo wangu miaka miwili iliyopita akiwa mtoto wa Mzee Masoud Abdulatif na mkewe wa Kiarabu, mzee mwekezaji aliyekuja Kibaha enzi hizo na kuwekeza katika sekta ya ujenzi… SASA ENDELEA..

Alikuwa akimiliki nyumba kadhaa zilizokuwa zimekodiwa na wafanyabiashara mbalimbali eneo la Kibaha. Salehe alikuwa kitinda mimba wa Mzee Masoud, mboni ya Mzee Masoud kwa vile tu alikuwa mtoto wa kiume pekee kwa mzee huyo kati ya wanawe wanne.

Nilimjulia Salehe baada ya kurudi kwao akitokea masomoni Uganda. Mzee Masoud alikuwa na tanki lililokuwa nje ya nyumba yake na mara nyingi mpwae Kianga ndiye aliyekuwa akisimamia mradi wa kuuza maji kwa kutumia tanki hilo. Mara chache jioni Salehe alipenda sana kumsaidia Kianga kusimamia uuzaji maji na hapo ndipo nilipomfahamu na siku ile ya kwanza tu ya kumuona nilikiri pamoja na dhiki zangu huyu ndiye mume wangu niliyeandikiwa na Mungu. Nilimpenda papohapo!

Hakuwa mwongeaji hili lilifanya watoto wa kike tupishane, tujishaue, tujichetushe kupitiliza ili japo atusabahi. Kila mmoja alitaka Salehe amuone yeye ndiye bora, kila mmoja alitaka Salehe amsalimie japo amtabasamie, ilikuwa vurumai, mechi isiyo na jezi wala mwamuzi. Tulipigana vikumbo nyumbani kung’ang’ania kwenda kuchota maji, tukapigana vikumbo mtaani mbele ya kijana huyu jamali, mwenyewe alikuwa kimya akitutazama tu!

Watoto wa matajiri wenzie akiwamo huyu Raya Khalfan mtoto wa mkurugenzi wa kiwanda cha fenicha kibaha, walipishana na magari wakiingia na kutoka nyumbani kwa Masoud. Watoto wa maskini tukamvizia bombani na kama ilivyo maskini huwa hachoki!

Katika kukua kwetu tumepitia suluba nyingi za kimaisha, yote kwa yote tuliyopitia mama yetu Mwanahamisi Mbegu hakuturuhusu kukata tamaa. Tulifunzwa kupigania kitu mpaka mwisho wa siku, iwe kwa njia halali au haramu ilikuwa lazima upate utakacho vinginevyo tulinyanyua mikono juu ya kushukuru kuwa lililotushinda halikuwa rizki ya kulika na kumezeka! Lakini kikubwa kuna nyakati wana wa Msasambuko tulijaaliwa umoja!

Heka heka za kumpata Salehe zilipamba moto zaidi mtaani kwetu baada ya baba yake Mzee Masoud kumnunulia gari dogo la kutembelea, tulizuzuka na ile vitara kupitiliza. Na   Maneno yakawa mengi mtaani mabinti waliomkatia tamaa na vijana wenzie wa kiume walimzushia mara alikuwa si rizki, mara alikuwa na mke marekani, mara alikuwa na mchumba wa mtoto wa waziri mradi yalizuka mema kwa mabaya juu yake.

Kikubwa alijiheshimu hakuna aliyebahatika kujigamba kumpata seuze kupata dakika chache za kusemezana naye faragha. Mbio zote na mbwembwe ziliishia bombani kwa Kianga!

Ni Jioni hii yenye bahati yake, ndio jioni hii iliyozaa safari ya haya yote yaliyoanzia bombani nikikinga ndoo zangu huku nikiitazama saa kila dakika, nakumbuka vizuri ilikuwa Jumamosi. Nilikuwa na haraka zangu, haraka ya kuwahi kurudi nyumbani kulikokuwa na ugeni rasmi.

Dada yangu aitwaye Semeni alikuwa akitolewa mahari na hivyo kulikuwa na shughuli kubwa ya kuhitajika huku na kule ili mambo yaende kama yalivyopangwa. Nikiwa nimesimama pembeni kabisa nikiitazama foleni ya ndoo ikisogea polepole, Kianga alikuja upande nilipokuwa nimesimama  na kunitaka nimsaidie kuhesabu sarafu nyingi alizokuwa nazo katika mfuko wa plastiki.

Tukaketi katika mfuniko wa chemba la duara kubwa lilikokuwa hapo kando na kuanza kuhesabu. Tulikuwa tukihesabu huku tukiongea hili na lile na kutaniana kusikokwisha.

‘Hivi ni kweli Semeni anaolewa?’ Akanitupia swali na kunikatisha kazi ya kuhesabu zile sarafu. Nikamtupia jicho la haraka ya kukubali kwa kutikisa kichwa. Kianga akatabasamu na kuchombezea.

‘nilimpenda kweli dada yako ila si mbaya nitampata Farida’ Kianga akatania akimtaja dada yangu wa sita Farida Msasambuko wenyewe mtaani wakimuita tanki la Kiboko kutokana na kujaaliwa makalio makubwa yaliyowakosesha usingizi wanaume wengi wa pale Kibaha Mzani.

Si madereva wa magari makubwa wala utingo wa mabasi ya mikoani walimjua Farida Msasambuko na mara kadhaa dada alisafiri mpaka mikoani bure kutokana na kupapatikiwa na wanaume lakini cha maana alichokuwa akikipata pamoja na uzuri wake wa haja ilikuwa ni kuzalishwa watoto wa baba tofauti kila mwaka. Mama yangu akakiri mwanae alipewa uzuri wa mwili akanyimwa akili! Akili ya maisha!

Wakati nikikaribia kumalizia zile hesabu, ndoo zangu zilishajazwa maji, Kianga hakunilipisha akaniachia ile hela kama msaada wa mahesabu madogo niliyomsaidia. Wakati nikisimama na kukukung’uta makalio yangu kuondoa mchanga nilimuona Salehe!

Alikuwa akija pale nilipokuwa nimesimama na Kianga. Nilitamani aongeze mwendo na kunifikia kwa haraka lakini wapi, alitembea kwa mwendo ule ule huku akionekana dhahiri kuchotwa na mazungumzo toka katika simu iliyokuwa sikioni mkono wa kuume hali mkono wa kushoto aliuzamisha kwenye mfuko wa suruali yake na mara kadhaa aliutoa na kuupitisha kichwani taratibu kuanzia utosini akizichachafya nywele zake za kimanga na kuutuliza mkono huo shingoni. Alivutia… Alipendeza!

Itaendelea Jumatatu…

Previous articleSIMU NI SUMU AU SUKARI YA PENZI?
Next articleMIDO FUNDI
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -