Saturday, November 28, 2020

ZUENA BINT MSASAMBUKO (5)

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA LAURA PETTIE,

ILIPOISHIA IJUMAA… Akanisindikiza mpaka karibu na nyumbani na kuniacha nimalizie umbali mdogo uliobaki. Nikiwa mnyonge kupitiliza niliingia ndani na kumkuta mama anahangaika kuwasha taa ya chemli. SASA ENDELEA…

‘Umeme hakuna?’ nikamuuliza mama nikihisi kuanza kukereka tena.

“Upo ila luku imekwisha na ni zamu yetu kununua, kaja hapa mwenye nyumba kanisemea maneno ya ovyo kweli,” mama akalalamika akinitazama kana kwamba mimi ndio niliyemsemea hayo maneno ya ovyo.

“Sasa umempa hiyo hela ya luku?” nikamuuliza nikianza kuchapua hatua kuelekea chumbani nisingoje hata jibu lake. Nilikuwa na yangu tani kwa tani kichwani. Nikamsikia mama akiongea kwa ghadhabu na wala sikumfuatilia.

Nikaifuata ile pochi iliyokuwa na pesa na kwenda nayo kitandani. Nikatoa bahasha ya kaki na kuzihesabu pesa zote. Zilikuwa elfu 90! Pungufu kumi… nikahesabu tena na tena. Hamaki na hasira vikanishika kwa pamoja. Nikachukua elfu 10 na kuharakisha kurudisha zile pesa bahashani kisha mbio nikatoka chumbani mle kwa hasira.

‘Wameshaniibia mama….’ nikampayukia mama ambaye wala hakugeuka kunitazama

‘Maisha gani haya mama… hela niwatafutie na kuniibia mniibie maisha gani haya… watu hamna shukrani humu ndani…nazunguka huku na kule kuwatafutia hela ya kula na bado mnaniibia jamani….naitaka elfu 10 yangu!…’ niliongea kwa uchungu machozi yakianza upya kunijaa machoni. Kamasi nyepesi zilirudi upya na kunisumbua kuzivutia ndani kila sekunde. Mama akaachana na ile chemli na kunitazama, akiwa amenishikia kiuno.

“Sasa unanipayukia mimi ndio nimechukua mwanangu?” akaniuliza kwa sauti ya upole iliyojaa masikitiko.

“Wanao ndio wameniibia….na nilishasema kikipotea kitu tena humu ndani nawasweka polisi.”

“Ukawasweke ndugu zako polisi kwa elfu 10?….hebu temea mate chini juu yatakurudia…uwazoe wenzio mpaka polisi kwa elfu 10?” mama akaanza kunijia juu.

“Kama elfu 10 ndogo wamewahi kuiokota barazani hapo?… nimeshachoka mama ….nimechoka wallah…mfanye mfanyalo kila mtu alete hela ya kula humu ndani, biashara ya kutegemeana ife, mi sina kazi tena…msinifuate na shida zenu tena…hela hiyo ya umeme ndio mwisho utajua na wanao wezi unaowatetea kila siku….kila mtu abebe mzigo wake sasa,” nikaongea kwa hasira machozi yakinitoka bila kikomo. Mama akanitazama katika namna ya kugundua machozi yale yalikuwa ni zaidi ya kuibiwa ile elfu 10. Akatulia akinitazama kwa masikitiko.

Nikarudi chumbani nikilia kama mtoto, na kuihamisha ile bahasha yenye pesa. Nikakaa kitandani mikono ikihangaika kuzuia kelele za kilio na kubana pumzi kujinyamazisha. Moyo ulikuwa unaniuma, moyo ulikuwa ukiteketea kwa moto wa maumivu.

Nikapeleka mkono wangu uvunguni na kuvuta boksi kubwa lilikokuwa na vitabu vyangu, madaftari na makaratasi kadhaa nikalipekua na kutoa bahasha ndogo ya pinki. Nikaifungua na kuchomoa kadi iliyokuwa na maneno Happy Birthday, nikaifungua kadi ile na kuitazama picha iliyokuwa katikati ya kadi ile. Picha ya Salehe Masoud, Salehe wangu….mikono ikahisi kutetemeka, moyo ukahisi kuwaka moyo. Maumivu! Yasiyoandikika karatasini wala kusomeka mdomoni yakapita kama kisu cha moyo ndani ya moyo…

Nikalia na kulia kisha taratibu nikatulia na kuyatuliza macho yangu katika ile picha. Masikio yangu yalihamia nje, kwa takribani dakika chache akili yangu ilitulia ikiusikiliza muziki mwororo uliokuwa ukitokea katika baa ya jirani, sikuweza kuutambua akilini wimbo ule lakini niliusikiliza  kwa majonzi, sauti tulivu ya mwanamuziki yule, vinanda na mirindimo ya polepole iliyosikika vema masikioni mwangu ilinifanya nifumbe macho yangu na kuruhusu machozi yatiririke taratibu mashavuni mwangu ilhali nikijaribu kutabasamu katikati ya huzuni hii.

‘Salehe…hivi kweli?…’ nikamtaja, nikajiuliza, nikivuta pumzi na kuzishusha taratibu. Nikakumbuka vizuri mahusiano yangu na Salehe, nikakumbuka vizuri migogoro yangu na Raya, nikamkumbuka vizuri Madobe Fungamlango, mpenzi wangu tangu utoto….lakini yote tisa kumi ni hili tukio lililokuwa mbele yangu, ningelikabilije?!

Mlio wa simu ukanitoa mawazoni, nikaitazama ‘screen’ zilikuwa namba za Vodacom ngeni kabisa. Nikajishauri kwa dakika kadhaa kabla ya kuipokea huku mawazo yangu yakichanganua simu ile ilikuwa ya nani. Nikahisi atakuwa Salehe pengine alitaka kuniaga, pengine alitaka kukutana nami tuzungumze. Nikahisi faraja. Nikatabasamu na kuipokea!

“Hallo mama, vipi?” sauti isiyo ngeni ikasikika upande wa pili kwa upole na unyenyekevu fulani. Nikafinya uso na kuguna

“Nani mwenzangu?’ nikauliza mkono wa kushoto ukigonga gonga kifua kujituliza.”

“Madobe mpenzi, simu haina hela natumia ya jirani hapa, sasa vipi?” Ilibaki kidogo niibamize simu ukutani. Yaani nilikereka tani zote za kukereka. Nikatamani kusonya nikashindwa.

“Vipi nini?” nikamuuliza hali nikimeza mate na kupumua ili kuji ‘control’.

“Zuena kwani tumeongea nini mchana mama?…mbona unanifanyia hivi mwenzio?… naona  kama nakukera kila ninapokupigia,” akalalamika na badala ya kumuonea huruma nikajikuta nazidi kukarahika. Nilikuwa na shida zangu, nilikuwa na maumivu yangu, nilikuwa na mizigo yangu! Nikatulia tu nisijue nimjibu nini.

“Zu!..” akaita.

“Nitakujulisha asubuhi Madobe, muda huu akili yangu haiko sawa,” nikamjibu polepole nikitaraji angekata simu na kunipa uhuru wa kukipumzisha kichwa.

“Iwe asubuhi basi mpenzi, maana mama atakuwa Muhimbili saa nane mchana, nataka nimtafute mtu wa kuzifuata huko asubuhi,” akajieleza kana kwamba nilishamhakikishia kuwa ningempatia. Umaskini ukizidi kidogo hicho mtaibiana, mtadaiana, mtang’ang’aniana na kukabana. Sikumjibu nikamuaga na kuikata ile simu. Kichwa kikiwa kizito kupitiliza! Umeme nao huo ukawaka!

….Sikumbuki nililala saa ngapi na kama hata nilikula chochote jioni ile, nilikurupuka saa moja asubuhi  baada kuhisi mtu akiniita kwa mbali. Nikalitoa shuka nililokuwa nimelitupia mpaka utosini na kukigeuza kichwa kumtazama msemeshaji, alikuwa mama. Nikaamka mzima mzima na kuketi, nikipiga miayo na kuizuia kwa kiganja cha mkono wa kushoto. Nikamsabahi.

Akanitazama tu asiitikie hata ile salamu zaidi ya kuyatanua macho yake na kuyaelekeza pembeni huku akikusanya midomo yake mithili ya mtu atafunaye kitu kichachu, akaja taratibu na kuketi pale kitandani akiendelea kunitazama. Akatikisa kichwa huku akiyahamisha macho yake na kutazama sakafuni akatulia kwa sekunde kadhaa. Akanigeukia.

‘Umetoka hapa jana ukarudi na kisirani cha Kimasai na hasira za Kihehe na ile hela kuibiwa basi ndio ukajiapiza kwa miungu ya Kizaramo….haya vipi?…maana hukula wala hukutaka kusemezana na mtu…kuna nini?’ mama akaniuliza kwa upole huku akinitazama kwa kituo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -