Saturday, November 28, 2020

ZUENA BINT MSASAMBUKO (7)

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA LAURA PETTIE,

ILIPOISHIA jana…. Baada ya kupata staftahi nikarejea chumbani na kuketi kitandani, nikikumbuka maombi ya Madobe. Nikampigia simu na kumtaka atume mtu aje kuchukua zile pesa. Niliamua kumpa potelea mbali nikiishiwa hata mia…

SASA ENDELEA…

Madobe Fungamlango alikuwa mpenzi tangu nikiwa darasa la sita, kabla hata sijachezwa unyago nilishayajua mapenzi moyoni, nilishajua kupenda ni kitu gani bahati mbaya baada ya kutoka ndani mwanaume wa kwanza akawa mpangaji mwenzetu mmoja ambaye alikuwa akinifadhili mahitaji madogo madogo. Watu husema eti mwanaume wa kwanza hasahauliki, ujinga gani huo! Huyu binadamu hata sura yake siikumbuki vema kichwani mwangu. Aliniingiza ulimwenguni humo nikazijua njia na chochoro nikachanja mbuga.

Hili lilikuwa pigo la kwanza kwa Madobe, alipojua aliumia sana, namaanisha sana kwani hakutarajia ila akasamehe yote akanipenda mara mbili ya mwanzo. Akiwa mtoto wa sita na wa kiume pekee katika familia yake, Madobe ni mpole, mpole mnooo, hajui kujibizana na mtu wala kugombana kwa namna yoyote.

Hajui kumchukia mtu wala kumfanyia visa. Hakuwa na uzuri wa sura ya kumtetemesha mwanamke lakini moyo wake ulikuwa kivutio cha kila mwanamwali. Bahati mbaya wanawake tumeumbwa kupenda sifa zinazoonekana bila kujali sifa za mtu zisizoonekana.

Nilipoingia kidato cha kwanza Madobe aliingia mitaani kufanya vibarua vya kila aina na mwisho wa siku alinipatia pesa nusu ya kile alichopata.

Hata kama kingekuwa kidogo kiasi gani. Alikuwa radhi alale na njaa yeye kuliko kuona nikiipitisha siku bila kula. Alipoahidi alitimiza ahadi zake. Ndio Madobe huyu bin Fungamlango, kijana aliyejitoa muhali kuona furaha yangu ikichanua hata kama ingekuwa ni kwa yeye kuwa chongo!

Hakuna ambaye hakuyajua mapenzi yetu, mpaka nyumbani walimjua Madobe. Nyakati nilizokaa nyumbani kusubiri karo Madobe alinitunza kwa hicho kidogo alichopata. Kweli kutoa ni moyo usambe si utajiri.

Na anayekupenda atajiweka rehani kwako asijali hali yako. Alinihimiza kusoma na alipenda nisome nifike mbali akidai alichukia umasikini ulioletwa na kukosa elimu, alijenga ndoto kadhaa za kuwa na watoto wachache waliosoma. Kilichomwangusha ni utegemezi wa familia yake kwake. Baada ya baba yake kufariki jukumu la kuitunza familia lilimgeukia yeye hivyo pamoja na juhudi zote pesa alizopata zilitumika mpaka senti ya mwisho!

Naikumbuka vema Ijumaa hii miaka miwili iliyopita, baada ya kutoka msikitini niliamua kwenda kwa subira kupiga soga na kupitisha muda. Nikiwa njiani akili yote ilikuwa kwenye simu niliyokuwa nayo mkononi.

Nilikuwa nikizungumza na Madobe kwa ujumbe mfupi, ilikuwa imepita wiki tangu familia yake ihamie Buza wakitokea huku Kibaha.

Wakati nikimpisha mwendesha baiskeli mbele yangu nikakumbuka nilikuwa nahitaji sindano ya kushonea, nikaiacha njia ya kuelekea kwa Subira na kulifuata duka. Yarabi! Salehe alikuwa pale dukani akitazama uelekeo ule ule niliokuwa nikitokea. Miguu ikaanza kujichanganya nisijue upi ulipaswa kutangulia.  Nikababaika!

Nadhani niligeuka kituko kwa sekunde kadhaa, nikalikaribia duka moyo ukipiga nusura utokeze nje ya mwili uliokuwa umelowa jasho ghafla. Kiwewe kilishanikamata, nikajitutumua kutulia na nisiweze! Waliosema kupenda maradhi ya moyo, hawakukosea. Nikamfikia alikuwa bado akinitazama bila kukwepesha hata macho. Loh! Aliniweza!

Nikamfikia pale alipokuwa na kuitafuta salamu ya kumpa nikakosa. Kichwa kilikuwa kitupu na ule mtandio kichwani nilihisi kama nimevaa kofia ya pikipiki, nadhani alitambua shughuli aliyokuwa ananipa akacheka uku akiinamisha kichwa, vile vijishimo vikajitokeza mashavuni mwake, meno yake yalipangana vyema yakaonekana sio mtu anakuchekea unahisi unaangalia mawe yanayozunguka bustani shule za msingi lile kubwa hilo dogo lile tofali hili donge la chokaa mradi tafrani tupu!

Uso wake jamali na macho yake matulivu yakafanya niwe zumbukuku mara mbili kipeo cha pili! Nilimpenda!

‘Zuena hivi kwanini unaniogopa?’ akanirushia mkuki moyoni na ukagota sawasawa. Nilitamani kumwambia Mangi dukani atoke nje japo anishikilie. Safari hii akacheka zaidi uku akitikisa kichwa.

‘Zuena!’ akaniita kwa sauti akijaribu kunitoa katika bumbuwazi. Ndio akili ikaanza kuitambua akilini manukato yake yale yale ya siku ile. Nikashuhsa pumzi na kuangalia chini nisiitike wala kujibu swali lake. Midomo ilikuwa ikinimwemweseka nikitamani nimtamkie yote ya moyoni.

Salehe akanisogelea karibu na kuushika mkono wangu wa kulia akiuteremsha chini toka mdomoni ulikokuwa. Nilikuwa nazitafuna kucha bila kujijua. Nikacheka! Na ukurubembe wote nilikuwa  nimepatikana!

‘Ulisafiri? sijakuona wiki hii nzima ukija kuchota maji’ akazidi kunisemesha nami nikizidi kupoteza muelekeo wa mazungumzo. Nikajitutumua na kuinua kichwa kumtazama

‘Nipo nimepumzika tu’ nikamjibu nikizivuta pumzi na kuzishusha, nikauma midomo yangu kwa pamoja ili kuituliza nafsi yangu. Nikaweza!

Simu yake aliyokuwa nayo mkononi ikaita, akanitazama kwa utulivu akinikazia macho yake mazuri, nikatamani nimkumbatie, nikatamani japo nimguse, nikatamani japo aendelee kusimama pale tuzungumze! Haikuwa bahati yangu akanitupia tabasamu na kuchapua hatua akitoka eneo lile na kulielekea gari lake uku akizungumza na simu yake….

Sikukumbuka kilichonileta pale dukani, nikakunja dera langu na kutoka mbio nikiishika njia ya kwenda kwa Subira. Nikitamani kupaa nimfikie Subira na kumsimulia ya leo. Njiani nilisimama nikawaza sekunde kadhaa na kujikuta nikicheka peke yangu. Salehe Masoud!

Ijumaa hii iliisha vema kupita ijumaa zote nilizowahi kuziona kabla. Nilihisi raha moyoni kupitiliza! Na matumani ya kumpata Salehe yakiongezeka, ila kitu kimoja tu sikukitilia maanani…je Salehe nafsini mwake alikuwa na hisia zozote kwangu? Sikuliona wala sikulifikiria wala sikulipa umakini jambo hili na sijui kwanini!

Mvua kubwa ilikuwa inanyesha, upepo nao haukuacha kufanya vurugu zake za hapa na pale ukiezua hiki na kutikisa kile. Nilikuwa nimejibanza kwenye jengo la posta ya zamani nikifikiria  namna nitakavyofika angalau Mwenge kwa shangazi yangu.

Nilitaka kulala hapo ili kesho yake niamkie kibaha badala ya kuminyana na watu kugombea magari ya ubungo na kisha nikapimane ubavu tena kuwahi magari yaelekeayo kibaha. Ilikuwa saa kumi jioni ila anga hili la wadidu liliutambulisha utusitusi uliofanya mng’ao wa anga utoweka na kuleta wingu zito lililoukaribisha usiku kabla ya muda wake.

Nikasonya zaidi baada ya upepo kuhamisha uelekeo wa mvua na kuuhamishia hapa tulipokuwa tumekusanyana kama fungu la kuni. Misonyo ikatutoka wengine wakilaani zaidi na kulalamika kusikoeleweka. Likaja daladala wenye mbio wakakimbizana na kusukumana mlangoni. Waliopanda walipanda na waliokwama wakarejea palepale.

Akili yangu ikahamia kwenye hiki kitu kilichonileta hapa posta. Biashara ya mama ntilie. Nilikuwa nimepata kibarua kwa mama mmoja wa kimanyema aliyekuwa anapika chakula cha asubuhi na mchana pale feri. Mama huyu aliwahi kuwa jirani yetu kule kibaha kabla ya kuhamia Magomeni makuti.

Maisha yalivyozidisha kitanzi nikamtafuta na wala hakuwa na hiyana akaniajiri. Na hii ndio ilikuwa siku yangu ya tatu tangu nianze hii shughuli iliyonilazimu kuamka alfajiri wa saa kumi na kufika nyumbani saa nne usiku. Ilikuwa biashara ya kuchosha ila angalau niliweza kuondoka na hela za maana kwa siku. Wenyewe tunasema Mwendaji si sawa na mkaaji!

Umati wa watu pale posta ulizidi, ukizingatia ulikuwa muda wa kutoka kazini, nikawaza cha kufanya, kwa sekunde kadhaa nilishuhudia watu wakipimana ubavu kwa kila gari lililokuja tena likiwa limejaa. Nikaona njia pekee ni kuyafuata magari yanapoanzia uko posta mpya.

Nikajitosa katika mvua nikiifuata barabara iliyokuwa inaelekea benki ya NBC. Nilijitanda upande wa khanga angalau kupunguza ile hali ya kulowana. Nikaifikia benki na kupita kandokando ya benki hii nikiikwepa mvua, nikakata kona na kuanza kuelekea ilipo ile sanamu ya Bismark!

‘Dada!…wee dada!’ nikasikia sauti nyuma yangu, nikatamani kugeuka lakini posta hapa na mvua hii nani wa kuniita mimi, au nimedondosha kitu, pengine hata sio mimi, kama ananijua si angeniita kwa jina langu, atajua mwenyewe…nikahitimisha hatua za mawazo yangu huku nikizidi kuongeza mwendo ili kulikaribia jengo lilikokuwa na ukingo wa kujikinga kando kabisa ya lile sanamu ilipo tawi la Benki la NMB sasa hivi.

Itaendelea kesho..

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -