Saturday, November 28, 2020

ZUENA BINT MSASAMBUKO (8)

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ILIPOISHIA jana… ‘Dada!…wee dada!’ nikasikia sauti nyuma yangu, nikatamani kugeuka lakini Posta hapa na mvua hii nani wa kuniita mimi, au nimedondosha kitu, pengine hata sio mimi, kama ananijua si angeniita kwa jina langu, atajua mwenyewe…nikahitimisha hatua za mawazo yangu huku nikizidi kuongeza mwendo ili kulikaribia jengo lilikokuwa na ukingo wa kujikinga kando kabisa ya lile sanamu lilipo tawi la benki la NMB sasa hivi… SASA ENDELEA..

Wakati nikilikaribia hili jengo walinzi waliokuwa kando karibu na jengo lile walinionyesha ishara ya kunitaka nigeuke nyuma. Safari hii sikupuuza nikageuka huku nikiishikilia vema khanga  niliyoikusanya chini ya kidevu. Nikatoa macho kwa bidii nikimtazama huyu kiumbe aliyekuwa umbali mrefu kidogo toka pale nilipokuwa.

Salehe Masoud! Akaniita kwa ishara ambayo kwa wakati ule wala sikuielewa! Nilikuwa bado nimesimama kwenye mvua na wala nisijitambue kama nalowana.

‘Unamjua?’ mlinzi mmoja akanitupia swali lililonitoa katika mshangao na bila hata kumjibu nikaanza kuchapua hatua za haraka haraka kumfuata Salehe.

“Nimekuona unapita hapo kwa kasi sana” akanisemesha mara tu nilipomkaribia huku akionionyesha kordo niliyopita. Nikatabasamu

‘Masalkheri’ nikamsabahi.

“Alkheri….njoo huku,” akaniamrisha nami kama kondoo nikamfuata nyuma nisijue hata ninakoelekea. Akanitangulia akielekea mbele ya jengo la NBC. Nikaliona gari lake, ile vitara yake. Akanigeukia ghafla akionekana kukunja uso kidogo.

“Si unaelekea nyumbani?’ akaniuliza

‘Ndio”,  nikajibu haraka haraka nikisahau na mipango yangu yote ya kulala  kwa shangazi. Ndio raha ya kichwa hakihitaji tume ya uchunguzi wala kamati ya utendaji ili kifanye maamuzi. Akaliendea gari lake na kunifungulia upande wangu wa kuketi mvua ilikuwa inamnyeshea nami bila kujali hilo. Nikajishaua!

‘Aah hapana Salehe nitakuloweshea kiti jamani, huoni nilivyolowa? Nikamuuliza huku nikimtazama alivyokuwa akizuia mvua isimpige usoni kwa kiganja chake.

‘Zuena Please!…’ akanibembeleza akiivuta hiyo please kwa madaha, mwenyewe mwili ukinisisimka, nikazidi kudengua!

“Asante bwana, nitapanda daladala tu’ nikajibaraguza huku moyoni nikitamani kutoka mbio na kujitupia ndani ya lile gari. Ila ndio hivyo mashauzi yalinijaa kama kuku kishingo!

Ghafla! Akaja haraka haraka pale nilipokuwa nimesimama na kunishika mkono wa kuume hali mkono wake wa kushoto ukizunguka mgongoni mwangu na kulikamata bega la kushoto! Almanusura nizimie! Akanikokota mpaka garini, nikapanda huku akinisaidia kuliweka sawa gauni langu refu  lisibanwe na mlango. Moyo ulikuwa unaenda mbio!

Akafunga mlango na kuzunguka mbele ya gari akaja upande wake na kufungua mlango, akajitosa na kuufunga. Tukawa wawili ndani ya gari. Akachomeka ufunguo na kuutekenya akipangua gia na kuanza kulirudisha nyuma. Nilitamani kugeuka mzimamzima na kumtazama vema ila ndio aibu zilifanya nikilaze kichwa changu kando na kutazama nje.

Tukaingia barabarani, safari ya Kibaha ikianza.

“Kwanini usiiondoe hiyo khanga?” akaniuliza taratibu akibonyeza bonyeza pale mbele ya gari na kufungulia Air Condition kwa mbali na kufungulia muziki. Nikaiondoa ile khanga na kuikunja. Nikalishika ziwa langu la kushoto, pochi yangu ndogo iliyokuwa na simu na hela ilikuwapo. Nikatulia!

Tulipoikaribia Mtaa wa Maktaba kukawa na foleni, nikashusha pumzi na kumtazama Salehe kwa kuibia. Alikuwa amekiegesha kichwa chake upande huku akikitikisa taratibu juu chini juu chini… mkono wa kushoto ukifanywa egemeo kwa tama ya ngumi.

Mkono wake wa kushoto ulinyooka na kulala katika usukani vidole vikigongagonga usukani ule kufuatisha muziki wa kizungu ulikokuwa unasikika polepole. Malaika kadhaa walilala vyema mkononi mwake kutokana na kule kulowa kwa mvua. Alinisisimua!

Taa zikaruhusu, gari likapinda kushoto kushika kuelekea barabara ya Bibi Titi, ukimya ulikuwa umetawala katika gari. Nadhani kila mmoja akiwa lake. Nilikuwa nikimtazama kwa kuibia mwisho kichwa changu kikachotwa na mawazo mengine.

Wakati tunaikaribia magomeni katika ile foleni nikageuza kichwa na kumtazama. Tukagonganisha macho!

Akacheka na kubadili stesheni  ya  redio iliyomleta mwanamuziki Diamond na kibao chake ‘nenda kamwambie’.

Akaonekana kuufurahia wimbo huo kwa kuongeza sauti maradufu. Nami nilikuwa naupenda huu wimbo nikajitutumua na kuimba sambamba na Diamond angalau kuvunja ule ukimya! Muda mfupi niliokaa naye ndani ya gari nilishaanza kumzoea. Akanitazama na kucheka kicheko cha sauti akifurahie vile nilivyomfuatisha Diamond.

Nenda kamwambie Jinsi navyo mpenda mi Na kama mapenzi bado Mwambie ntayaongeza mi Nasema kamwambie….’  tukaimba kwa pamoja kibwagizo hicho uku tukitazamana na kuangua kicheko cha pamoja.

‘Ana sauti nzuri sana huyu jamaa  aisee’ akamsifia

‘Saaana….’ Nikaitikia kishabiki mikono nikiifumbata kifuani.

‘Kama yako!’ akanitania

‘Aah wapi siwezi kumfikia’ nikakataa uku nikijichekesha bila mpango!

‘Huwezi kujijua…mimi ndiye ninayeisikia sauti yako…. sasa unabisha nini’ akanibana nisizidi kumbishia na aliweza nikamtizama kike haswa na kutabasamu ila Sikumjibu!

Foleni ilikuwa kubwa, lakini wala haikunikarahisha. Kuwa ndani ya gari lenye kiyoyozi na dereva nimuotaye kwenye njozi, hapana nitakuwa mnafiki nikisema sikuifurahia foleni ile. Nikazama tena mawazoni nikimkumbuka Madobe na meseji yake ya mwisho kwangu jioni ile…

‘Usifanye papara zisizo na msingi Zu wangu mambo yakikaa sawa natuma mshenga mwaka huu hauishi. Nikutakie jioni njema ukifika mwenge salama nipigie unijulishe mama’ nikautafakari ujumbe huo kichwani moyo ukihisi kusutwa na maizngira niliyopo. Shetani naye ana nguvu zake. Wakati nikimuwaza Madobe, nikamsikia Salehe akinitoa mawazoni.

‘Unawaza sana….kwanini?’ akaniuliza akipangua gia sasa tukiingia manzese na kulipita lile daraja.

‘Nimechoka tu’ nikamjibu nikimtazama pasipo kumuogopa sasa.

‘Njoo nikubebe’ akanitania nami nikacheka pasi kifani yeye wala akaweka akiba kicheko chake. Safari yetu ikaendelea tukitaniana, tukisemeshana na angalau nikimuuliza hili na lile kuhusiana na familia yake.

Na ndio nikamjua Salehe angalau kwa undani kiasi. Nikaijua familia na kuwajua dada zake kwa majina na mahali walipo.

Tuliingia kibaha saa mbili kasoro kutokana na foleni kadha tulizokumbana nazo huku na kule. Pilikapilika za hapa na pale mtaani kwetu bado zilikuwa zinaendelea na muda huu hakuna aliyekuwa na muda na mwenzie.

Kila mtu alionekana kuwa busy na kile afanyacho na safari za watoto za nenda rudi  dukani ndio zilikuwa nyingi uku vibatari vya wauza samaki vikionekana kwenye baadhi ya baraza za nyumba.

Nilijua pengine atanishusha njia panda ya kuelekea kwetu na yeye angeelekea kwao. Haikuwa hivyo aliniuliza uelekea wa nyumbani kwetu, baada ya kubishana sana nikamuelekeza. Sio kwamba sikutaka apajue nyumbani bali kwanza,  ile hali ya dhiki ya mazingira ya nyumba tuliyokuwa tunaishi yalinifanya nijisikie fadhaa kumpeleka.

Pili, maneno ya watu, japo si moto kwamba yataniunguza ila hawa wapangaji wenzangu na majirani kadhaa walikuwa na hekaheka na shughuli za vitanda na mikeka! Jambo dogo lingezua minong’ono wiki nzima. Sikutaka shari!

Akanifikisha mpaka barazani! Akina mama kadhaa waliokuwa barazani hapo wakiuza samaki shingo zikawasimama, wengine wachache waliokuwa kordoni almanusura waparamie majiko yao ya mkaa wakati wakihangaika kunyoosha shingo zao kulitazama gari na wasione hicho kilicho ndani! Uzuri umeme ulikuwa umekatika mtaa mzima!

Salehe alicheka! Maana wauza samaki nao walikazana kunyanyua makarai yao juu tayari kumkimbizia wakidhani mteja. Nikamshukuru kwa lifti na kumtaka radhi kwa ule usumbufu wa kunileta hku mpaka barazani kwetu.

Hakujibu! Alikuwa akinitazama  tu, nikagundua alikuwa akihema kwa nguvu kidogo wakati mwenzake shukrani zikinimwagika!

‘Hey Zuena’ akaita taratibu kwa sauti nzito kidogo, ikiwa na mikwaruzo iliyoambatana na pumzi zilizomtoka kwa nguvu uku akiupeleka mkono wake eneo la kiunoni changu. Hapana, nikaruka juu nikishtuka kama mtu aliyetekenywa.

Hakunigusa alikuwa akibonyeza kidude cha kufyatulia mkanda wa gari niliokuwa nimeupitisha kifuani. Nikajishtukia nami pumzi zikipishana kwa fujo puani! Nikajikuna kuna shingoni nikikwepa kumtazama usoni na kujifanya nikitafakari kitu!

‘Si ushuke na wewe kha!’ akili ikauambia mwili na mwili nao ukigoma hata kusogea! Kuna kitu nilitaka na sikujua ni kitu gani! Nikatulia na kumtazama kwa kina.

Alinivutia sana, alinisisimua kwa vile tu alivyo, nikajikuta naziweka aibu zangu kando na kukaribia nyuso zetu zikiwa mkabala mkono wangu wa kuume ukiufuata ubavu wake wa kushoto.

Itaendelea kesho…

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -