Thursday, December 3, 2020

ZUENA BINTI MSASAMBUKO (18)

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ILIPOISHIA JANA… Kiherehere kilinikaa moyoni, kwanini hapokei simu, yuko wapi….labda iko kwenye chaji, mh! Ndio asisikie hata mlio?…wehu ulinichekea waziwazi kwa ile hali kujiuliza kwa sauti na kujijibu. Mapenzi yasikie tu!.. SASA ENDELEA

Nikarejea chumbani na kujitupa kitandani, kwa dakika kama kumi nikatulia nikiwaza na kuwazua. Nikaishika tena simu na kupiga. Nikajuta na kwanini nilipiga… simu iliita kwa muda kisha ikapokelewa.

“Babe jamani uko wapi nakupigia hivi simu hupokei?”

“Babe wako nani?…..kwanza we nani? Sauti ya kike ikahoji. Macho yakanitoka nusura yanidondoke. Mdomo uliokuwa ukiongea kama cherehani ulibaki wazi usiweze hata kumeza mate

“Hallow….bibie we nani?” sauti ya yule mwanamke ilisikika ikihoji kwa ukali.

“Mscheeew!” akanitupia msonyo mrefu akimalizia…… “mkome kupigia pigia simu waume za watu, usiku huu hamna pa kujibanza huko mpaka msumbue watu usiku wote huu. Koma mwanamke!” simu ikakatwa. Nikazitazama namba nilizopiga zilikuwa za Salehe, namba zake ninazotumia muda wote. Nikaumia moyo, nikaumia jamani, nikaumia mno. Huku mikono ikinitetemeka, nikaamua kupiga tena, safari hii nikiandaa kupambana.

“Namba unayopiga kwa sasa haipatikani, jaribu tena baadaye,” customer care wakanipa jibu hilo.

Mwili ulihisi ganzi, ukahisi na maumivu kwa wakati mmoja. Moyo ukakamata hamaniko la kuhangaisha. Nikatafuta cha kufanya nisikione. Nikahisi kulia na machozi hayakuja, nilikuwa katika bumbuwazi.

Waume za watu? Saa nne hii? Yuko na nani? Na wapi? Mbona sijakosea namba?…. ina maana Salehe ananizunguka?….ina maana ananichezea akili?…nahisi mkuki moyoni, nikajaribu kuandika meseji mikono ilikuwa ikitetemeka, nikaiweka simu chini nikilala kiubavu na kujikunyata, nilihisi kuumwa ghafla, Salehe! Kutahamaki machozi yalikuwa yananitiririka bila kujitambua…..nimechoka sasa! Nini hiki?….niseme tu nilihamanika kupitiliza na aliyewahi kupitia hamaniko kama hili anajua nilivyojisikia!

Haya shughuli ndio imeanza kama ni pilau basi ndio tunapembua mchele!

*******

Sala ya alfajiri ilipoanza nilikuwa macho, sikufunga hata ukope, moyo ulikuwa na jitimai, maumivu ya hali ya juu. Nililala nikimuwaza huyu binadamu, niliwaza nikiumia nilivyojitoa kirahisi tu na kisha kuanza kukumbana na madhila  kama haya. Niliumia si utani!….kuna nyakati nawaza moyo umeumbwa kwa “material” gani kiasi cha kustahimili dhahama kama hizi.

Ilikuwa siku ya kazi, ilinipasa nidamke alfajiri hiyo na kujiandaa, changanya na baridi ya alfajiri ile nilikuwa kama mgonjwa wa homa. Saa moja kasoro nilikuwa posta nikisukuma chapati na kuzichoma. Bosi wangu alikuwa na shughuli ya kuchoma maandazi, huku msaidizi mwingine akitengeneza sambusa za viazi. Biashara ilikuwa ya ushindani kutokana na akina mama wengi kuwa na biashara moja katika eneo moja.

Ajabu ya Mola, banda letu lilijaa watu si asubuhi si mchana. Tukaanza kutuhumiwa kutumia uchawi. Haikuwa hivyo, tulijua wateja wetu walihitaji vyakula vyenye ladha ya kuvutia kama chai yenye tangawizi, maandazi yenye iliki, huku bosi wetu akijitahidi kuweka mazingira katika hali ya usafi wa hali ya juu, tukigawa tishu baada ya kunawa na sehemu yetu ya kupikia ikiwa safi mno.

Ila kikubwa ni uchanganfu wetu kwa wateja. Tulikuwa watatu tu, lakini wenye spidi ya ajabu, na kwa wale wateja wa kila siku kuna wakati tulilazimika kuwapelekea chakula maofisini mwao. Kazi hiyo ikawa yangu.

Saa mbili na robo nilikuwa kwenye lifti nikielekea ofisi moja uko ghorofani kupeleka chai na vitafunio kwa mteja wetu mmoja aliyekuwa Meneja wa hiyo ofisi. Nikafika ofisini pale na kumkuta sekretari ambaye alishanizoea na alikuwa tofauti na masekretari wengine wenye nyodo za “una shida gani”, huyu alikuwa mkarimu sana. Akaniruhusu nikamuone meneja ofisini baada ya utani wa hapa na pale.

“Mchana utakula nini?” nikamuuliza nikitabasamu.

“Kuna menyu gani leo,” akauliza, akionekana kufurahia harufu nzuri ya chai niliyommiminia na chapati zilizokuwa mbele yake.

“Wali maharage na kabichi kwa samaki mkavu, nyama au maini, pilau, ndizi, ila ugali una dagaa, matembele na mlenda pia,” nikamtajia menyu naye akatafakari kidogo na kunijibu:

“Niletee ugali dagaa na matembele, niwekee na kipande cha pilipili,” akatoa oda yake nikiiandika katika karatasi. Huyu alikuwa mteja wangu wa mwisho kumpelekea chai, hivyo nilitoka pale nikinyoosha moja kwa moja kwenda kibaruani kwangu.

Wakati nikitoka ndani ya lifti na kuanza kukanyaga mguu kuuendea mlango mkubwa wa kutokea nje, nikasikia mtu akiniita tena jina langu na akija mbio kweli. Nikageuka, alikuwa Salehe! Sikusimama, nikanyoosha na kutoka nje haraka mno. Sikutaka hata kugeuka tena, nikapiga moyo konde na kukaza mwendo nikivuka barabara na kuchapa mguu. Nikafika kazini moyo ukinienda mbio. Simu yangu iliyokuwa kwenye mkoba wangu ilikuwa imezimika.

Nikaiwasha nikianza kugundua simu yangu ilikuwa na matatizo ya kuzimika bila sababu. Meseji 8 zikuwa zimeingia, huku 5 kati ya hizo zikiwa za Salehe. Nikatulia kwanza na kutafuta mkao wa kuzisoma zile meseji. Zote zilihusu “missed call” zangu za jana, akijitetea simu ilikuwa kwenye chaji. Mpuuzi huyu! Na ndiyo kusema ile chaji ndio ilinijibu vile tena saa nne usiku!

Nikacheka kwanza nikijihurumia! Huyu atanitia wazimu wa bure, nikamuweka kando. Na siku hii nikamuomba mwenzangu asambaze chakula cha mchana, nikiogopa kukutana na Salehe ndani ya lile jengo.

Itaendelea Jumatatu

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -