Tuesday, November 24, 2020

ZUENA BINTI MSASAMBUKO (19)

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ILIPOISHIA Jumamosi…. Nikacheka kwanza nikijihurumia! Huyu atanitia wazimu wa bure, nikamuweka kando. Na siku hii nikamuomba mwenzangu asambaze chakula cha mchana, nikiogopa kukutana na Salehe ndani ya lile jengo…SASA ENDELEA

Nilichapa kazi zangu, zilipoisha nikampigia Madobe simu, tukaonana ubungo, tukitafuta mahali na kupeana raha akiniletea na ile 30,000 aliyoniahidi jana yake. Tukaagana roho zikiwa zimetulia kwa vicheko na bashasha. Alipiga simu akachoka, alituma meseji asijibiwe hata moja. Nikaingia Kibaha saa mbili usiku na vichapo kadhaa nikapita kwanza kwa Subira. Nikamsimulia mkasa mzima wa jana yake. Subira akacheka sana, akinitazama toka juu hadi chini.

‘Unaumia nini? Aliyekwambia Salehe shirika la misaada nani mpaka atoe tu asipokee?…. ndio ilibidi ulipie ulivyochukua shoga, dunia ya leo nipe nikupe, toa upate mjanja ni yule mwenye vyake’ akanishushua akiendelea kunizodoa.

‘Na unamuendekeza mno, hebu muweke kando kwanza atakutumia kama kijiti cha meno kisha akutupe kule…. Sikatai ana hela nzuri ila moyo wako umempenda kwa dhati ndio tatizo hilo, unayempenda huwezi kumchuna kisawasawa, we kama unachuna mchune kwa roho ngumu bila kutazama usoni hivi hivi utampa bure na mwisho wa siku ukose vyote,” Subira akazidi kunisokomezea ukweli, mimi kimya nikitafakari yangu!

‘Moyo hauna adabu Zuena ukiuendekeza utakupelekesha!…..mwanaume gani kila siku akuweke roho juu, kila siku akulize bila sababu, kila siku ukumbwe na majinamizi ya wanawake na ukute ni yule bibie mliyepimana ubavu siku ile na ukute naye alibembelezwa uko akadanganywa akatulia……hahahahaaaa mwaka huu wako!’ Subira akanyuka pale alipoketi na kumsaidia mumewe kuingiza cherehani ndani. Nikaga na kuondoka.

Wakati nakaribia nyumbani pale ilishatimia saa 3 nikaliona gari la Salehe.  Nikaguna nikiibetua na midomo yangu. Nikalifikia na kumkuta ameliegemea gari lake akiongea na Yasinta mpangaji mwenzetu aliyekuwa anapepeta mchele hapo nje, sikumshangaa maana  nyumba zetu hizi watu saa tano usiku ndio unasikia harufu ya dagaa wakikaangwa! Wakati mwingine unasikia harufu ya pilau inaambaa ambaa saa sita kasoro usiku.

Nikawasabahi na kuwapita nikielekea ndani. Nikamsikia vizuri alipokuwa ananiita, sikugeuka wala kuitika. Nikazama ndani. Nikifikia chumbani na kujitupa kitandani.

Akanipigia simu sikuipokea mpaka ilipokatika yenyewe. Nikatoa gazeti la udaku nililonunua siku hiyo na kuanza kulisoma nikiwa nimelalia mgongo. Simu yangu ilikuwa inaita mfululizo, nikajionea tabu, nikaizima!

Nilitaka kwa dakika kadhaa ajue kumpenda isiwe tabu wala sababu. Kwa asilimia mia moja alikuwa na mwanamke jana. Kilichoniuma zaidi ni kuwa alikuwa nami jioni ya siku hiyo na usiku wake akawa na mwingine.

Laanakum! Ewe mwanamke mwenzangu hata siku moja usije ukakiamini kiapo cha mwanaume hata akijiapiza kwa jina la mama yake mzazi tena kiapo kinachotoka kitandani. Usimuamini! Narudia usimuamini! Tunaponzwa na mioyo yetu miepesi kusamehe na kuamini lakini kwa dunia ya leo inapobidi lazima uuweke moyo pembeni na utumie kichwa kufikiri! Hujanielewa?

Wakati nikiwa nimetopea katika gazeti langu mama na Semeni wakaingia mle chumbani.

‘Nasikia Salehe alikuwa hapo nje’ mama akaniuliza

‘Nilimuona hapo nje wakati nakuja’ nikamjibu

‘Sasa umeshaongea naye maana muda huu Yasinta akaniambia alikuwa bado kasimama hapo nje’

‘Mi nimetoka kazini nikamsabahi hapo nikaingia zangu ndani….sijui shida zake’ nikajibu nikilikunja gazeti na kulivuta lile boksi chini ya uvungu, nikalitupia humo. Semeni aliyekuwa anamnyonyesha mwanae akiwa ameketi pale kitandani, akanigeukia na kunitazama akikunja uso kidogo kuonyesha kushtushwa na hilo jibu. Achilia mbali mguno alioutoa mama wakati ule.

‘Mmeshagombana tena?’ mama akahoji akiuelekea mlango wa chumbani na kuufunga vizuri. Akarudi na kuliondoa tenga lililokuwa juu stuli kando ya kitanda na kuichukua ile stuli. Nikatulia kwanza nikipisha kashda za mama kisha nikamsimulia kila kitu. Mama akasikitika sana, akinikumbusha maonyo yake!

‘Hakuna mwanaume kama Madobe! Hawa madishikonda watakupa ugonjwa wa moyo bure…’ Semeni akaniambia kwa upole.  Tukajadiliana hapo wakiniachia uamuzi wa mwisho mwenyewe. Tukarudi kwa Semeni sasa, alikuwa amekuja kufuata hela kidogo ya mahitaji ya shule ya Shidazangu aliyekuwa anaishi nae kwa wakati huo. Mumewe mambo yake hayakuwa mazuri na pia alikuwa akisumbuliwa na miguu hivyo ulezi wa familia ulimuelemea. Walikuwa na watoto sita, mumewe akiwa na watatu aliowazaa kabla ya kumuoa Semeni, Semeni nae akiwa na wawili aliowazaa kabla ndoa na sasa walikuwa na mtoto wao. Maisha yalikuwa magumu, Semeni akitegemea vibarua vya kulima kila siku ili familia ipate mahitaji katika kipindi hiki cha ugonjwa wa mumewe. Alihitaji msaada!

Nilimuhurumia sana, alikuwa amepungua na hata ule uzuri wake ulikuwa umechujuka mno. Alimpigia Shabani simu akajibiwa ngoja nizungumze na mke wangu, na ndio mwezi ulishakatika bado alikuwa anazungumza na mkewe. Jibu alishalipata kuwa asitegemee kupata msaada. Akakusanya nauli na kuja nyumbani kuomba msaada wowote hata wa chakula. Wakati huo huo alihitajika kurudi kwake  haraka kwani alikuwa amemuachia Shidazangu mji. Tukajadiliana sana ikabidi nitoe laki moja kumsaidia dada yangu. Mumewe apate tiba, mahitaji ya Shidazangu, chakula na mengineyo. Kweli laki si pesa! Dada Semeni akaipokea uku akitoa machozi. Akinishukuru kupitiliza.  Nikamchagulia na nguo zangu chache na kumpatia. Nikamfuta machozi na kumkumbusha kuwa nilikuwa mdogo wake na niliwajibika kumsaidia kwa kiwango kilicho ndani ya uwezo wangu.

Ndio maskini tunavyozidi kuwa maskini kwa kuzungukwa na maskini. Ukizipata kidogo hazikai kama si kwa shida yako basi ya shida ya mwenzako.  Sikuwa na roho ya choyo wala sikuwa na roho ya umimi. Nilichopata nilitumia na ndugu zangu.

Wiki nzima nilifanya shughuli zangu kama kawaida, nikiyaondoa mawazo ya Salehe kichwani. Alinitafuta kadri alivyoweza nami nikamkwepa kwa kadri nilivyoweza mpaka jumamosi hii niliyowahi kurudi toka mihangaikoni mwangu na kuamua kufua nguo kule uwani. Ilikuwa nikakione kiwanja changu ila Madobe alipata safari ya kikazi. Nikatulia nyumbani….kule uwani nilikuwa na wapangaji kadhaa tukiongea na kucheka. Tulikuwa tukimsema mama Abui alivyopata jakamoyo baada ya kumuona Semeni vile alivyokuja.

Semeni alikuwa anamnyima raha sana lakini dada hakuja kwa makuu, alifuata msaada na wala hakuangaika na Mzee Abui ambaye alitakiwa kumsaidia kulea mtoto aliyezaa nae. Dada hakutaka kuanzisha sokomoko!

Baada ya kufua na kuanika, nikapumzika barazani pale nikimuita na mpaka rangi mmoja anipake rangi miguuni. Nilikuwa nimefunga khanga yangu kifuani, khanga moja tu na nguo ya ndani basi. Na jinsi nilivyokuwa nimeikusanya ile khanga katikati sehemu kubwa ya mapaja yangu  maangavu aliyoshiba nyama ilikuwa nje. Mpaka rangi mwenyewe alikuwa akihangaika nami rohoni nikicheka peke yangu. Nilikuwa nimekaa pembezoni bega langu la kushoto likiegemea ukutani, upande wangu wa kulia  mita chache alikuwa ameketi Yasinta akimsuka Maria mtoto wa mpangaji mwenzetu. Wapangaji wengine walikuwa wametoka kila mtu na safari zake.

‘Wakubwa wanafaidi jamani; akasema mpaka rangi akikazana kunifuta ile rangi ya zamani

‘Wanafaidi nini na wewe hebu fanya haraka acha kuhangaika’ nikamshushua

‘Ana maneno huyu kama gazeti’ Yasinta akamtania

‘Kwani nasema uongo jamani, mipaja hii ukiipatia nafasi halafu ukajilia chipsi kavu tu wallah unaweza kupata kifafa utu uzimani, mipaja kama hii lazima uwe umekula nguna la kutosha na viroba vya ukweli’ Mpaka rangi akayatathmini mapaja yangu, akituacha tunacheka huku tukimtaka anyamaze kuna watoto waliokuwa wanacheza jirani jumlisha na Maria aliyekuwa anasukwa. Akakana!

‘Kwani kuna watoto siku hizi?….aaaa wapi bwana kuna mtoto nilibebana nae mpaka gesti, nilijua mtoto maana mdogodogo, mambo niliyokuta humo nilivaa suruali zipu inaangalia nyuma….balaa! unaambiwa mtoto ana sarakasi sijapata ona nikaona nitakufa kifo cha aibu sikumuaga! Nilitoka mbio nikaenda kuvaa suruali vizuri choo cha stendi kule…’ tukacheka sana namna alivyokuwa akisimulia hizo sarakasi.

‘Mwehu wewe hebu nyamaza bwana’ nikamgonga konzi kichwani nikimtaka anyamaze huku nikicheka. Nilicheka nikikumbuka mengi ya utoto wangu. Wakati akimalizia kazi yake. Ghafla gari la Salehe lilisimama pale mbele akashuka na kunifuata pale nilipoketi kwa kasi. Hakunisemesha alimvuta yule mpaka rangi na kumdondoshea pembeni. Akiwa amekunja uso akaninyanyua ghafla na kunivutia kwenye gari. Nikapingana nae nikijaribu kuzuia ile khanga moja isinitoke mwilini.

‘Hebu niache uko we’ vipi?’ nikamkemea nikiunyonga mkono wangu na kutaka kuuondoa mkononi mwake. Hakunisikiliza na alikuwa na nguvu fulani zaidi yangu. Akalifikia gari na kufungua mlango.

Itaendelea kesho..

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -