Thursday, December 3, 2020

ZUENA BINTI MASASAMBUKO (21)

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA LAURA PETTIE,

Vile alivyokuwa akitoa maelezo yake ungetamani asinyamaze, alikuwa na tambo fulani kama wanawake weusi wa Kimarekani wanavyozungumza. Hapa sinema ilikuwa ya bure!

Shushu lile lilimuuuma Raya, akafura na haraka akaelekea kumfuata Judith ili kichapo kitembee na ndio Salehe ambaye sasa alikuwa ameketi kwenye sofa kubwa akanyayuka na kunyooshea mkono Raya mithili ya trafiki anayesimamisha gari na kumpunguza kasi Raya! Pale aliposimama Salehe kulia kwake alisimama Judith kushoto kwake alisimama Raya na mimi nilikuwa nimeketi kwenye kochi  mbele yake.

‘SIWAELEWI!’ Akatamka kwa ukali huku akitikisa kichwa, mikono yake akiipeleka mfukoni mwa suruali yake, uso wake mtulivu ukionekana kujaa hasira na kuondoa ule utulivu niliouzoea usoni mwake.

‘Hii ni nyumba yangu! Kinachowafanya mpigizane kelele hapa kwangu ni nini?’ akatuuliza kwa ukali. Akamnyooshea kidole cha shahada Raya kwa mkono wake wa kushoto.

“Okay naanza na wewe chukua takataka zako na uondoke haraka,” akamkemea akiwa amemkunjia uso, akikiondoa kile kidole toka kwa Raya na kukihamishia katika maua na ile champagne yake. Nusura nicheke kwa sauti! Ile hamaki iliyoonekana usoni pa Raya iliniburudisha mno.

‘Nini?!’ Raya akauliza akibabaika na kumwemwesa midomo yake.

‘Babe! Nini kinaendelea hapa kwani?’ akamuuliza Salehe akimkaribia ili amguse. Salehe akamzuia na kumuonyesha mlango.

‘Salehe unanifanyia hivi?….kweli?….Salehe unanidhalilisha hivi mbele ya hawa malaya wako?’ Raya akalalamika machozi yakianza kumjaa machoni.

‘Shut up! Sipendi matusi ndani ya nyumba yangu….hebu kusanya vitu vyako uondoke bwana….namaanisha uondoke sasa hivi Suriama huyu akatamka kwa pozi akiyatuliza macho yake usoni pa Raya na kuachia tabasamu ambalo ni dhahiri lililenga kudhihaki ila kwa dakika hizi lilimpendeza mno. Nikatamani ayarudie yale maneno niyasikie tena na tena.

Raya akalia nami moyo ukafurahia kweli angalau ameyasikia maumivu niliyoyasikia wiki iliyopita.

‘Salehe!’ akatamka kwa huzuni kweli akiyaachia machozi yamchuruzike mashavuni.

Salehe akamfuata na kumshika mkono taratibu akimpeleka nje Raya hakubisha ila alikuwa akilia kwa kwikwii na kwa kiasi fulani nikahisi kuanza kumhurumia. Walipotoka mlangoni. Tukakimbizana  na Judith kusikiliza maongezi yao tukijibanza nyuma la mlango na kuchungulia nje kwa vile hawakuufunga!

‘Salehe unanifanyia hivi?’ akauliza akiwa haamini.

‘Raya! Nimetumia njia ya kistaarabu zaidi kukueleza hisia zangu juu yako…hutaki kunielewa, hutaki kukubaliana na mimi hutaki kunisikiliza kwanini?’

‘Kwa vile najua unanipenda na yule mchawi amekufanyia madawa Salehe….Zuena mchawi watu wote hapa Kibaha wanajua familia yao imejaa washirikina….Salehe moyo wangu’ …..mimi na Judith tukatazama tukiziba midomo yetu isitoe mshangao wa sauti, Raya alilia akikishika kifua chake.

Niliyahisi maumivu aliyokuwa akiyasikia muda ule. Ni mithili ya kuwekewa moto kifuani. Moyo huwa unauma vibaya hasa unapokutana na zahama kama hili. Kama umewahi kukutana na maumivu kama haya utakuwa unanielewa vema nini namaanisha.

‘Nenda nyumbani Raya! Huu si muda mzuri wa kuongea haya’ Salehe akamuasa akimshika mabegani na kuunyanyua uso wa Raya kwa kidole chake cha shahada.

Alimtazama machoni moja kwa moja, sie huku ndani tukisusuika, atambusu? Nikaiuliza nafsi yangu nadhani hata mwenzangu swali hilo lilimtembelea.

Salehe akatulia kwa dakika kadhaa akimtazama Raya machoni, akiyashuhudia machozi ya Raya yakimtoka. Akamtupia kifuani mwake na kumkumbatia.

‘Raya acha kulia basi mama’ akambembeleza sie uku ndani tusielewe nini kinafuata.  Mtu humtaki, umamtimua hiyo biashara ya kuwekana kifuani na kubembelezana inatoka wapi? Nikajawa na wivu nikitamani niwafuate hapo nje na kuwapa vidonge vyao asprin kwa panadol waachiane kila mtu njia yake. Nikavumilia kwanza nisijali hata hali ya mwenzangu uko ndani!

Akamtoa kifuani na kumsindikiza hadi kwenye gari lake, Raya akasimama akimtazama Salehe na kumsemesha kwa sauti ya kudeka, sikusikia alichomwambia ila Salehe alicheka na kuinamisha kichwa chini uku akikitikisa. Raya akarusha busu la kupeperusha na lisijibiwe. Akaingia garini na kuanza kuliondoa. Salehe alipohakikisha Raya ameondoka akashusha pumzi kama mtu aliyetua mzigo na kugeuka kurejea ndani.

Tukatoka pale nyuma ya pazia na kuketi sofani kila mmoja na sofa lake. Judith akiketi sofa alilokuwa ameketi Salehe na mimi nikirejea kwenye sofa langu. Salehe akausukuma lango na kuingia, akasimama katikati yetu akitutazama wa awamu kisha taratibu akaja kwenye lile sofa nililoketi akaketi pembeni yangu.

“Judy! This is Zuena nadhani umewahi kumuona…na…nina hakika mnajuana” akasema Salehe polepole akimtazama Judith aliyekuwa kimya akituangalia tu.

“Eeh…Zuena ..huyu ni Judithi ni best friend wangu,” akamtambulisha, akikwepa kumuita ex ama mpenzi wake wa zamani. Mradi nilishajua sikuleta papara.

“Nashukuru kumfahamu ingawa namjua kwa muda sasa sema jina lake nilikuwa silifahamu,” nikamjibu Salehe aliyeonekana kukosa amani kidogo. Judith akatabasamu.

“Sikujua wewe ndio uliyenipokea kijiti katika hizi mbio za mapenzi,”  Judith akabwaga manyanga na kumfanya Salehe atikise kichwa kwa namna ya kumkataza Judith asizidi kuongea. Too late!

“Salehe ni ex wangu….na kilichofanya tutengane sijajua mpaka leo labda nimuulize,” akasema Judith kwa kujiamini kabisa. Nikachoka!

“Judy please….mengine sio ya kuongea sasa,” Salehe akamuasa.

“No! kwani kuna ubaya ukimpa muhtasari anayeingia unakotoka?” akauliza kwa kebehi kidogo, nisielewe hata moja.

“Please Judy sikukupigia simu tuje kugombana please….okay sikukwambia kuhusu Zuena, nilikuwa nangoja wakati sahihi….si kwamba nilikuficha,” akajitetea Salehe. Mimi nikikosa hata nguvu ya kuuliza kisa cha kunitukana usiku ule ni nini. Niliacha ukweli ujianike wenyewe.

“Wakati sahihi?….wakati sahihi upi ilhali tulikutana kimwili usiku ule?…..wakati sahihi? Salehe?  So…. Mwambie Zuena ukweli na kama unamuoa mwambia fika kuwa She will keep the ring and I”ll keep the husband! (atatunza pete mimi nitatunza mume),” akanyanyuka na kunyakua pochi yake kochi la pili achapua hatua kadhaa kisha akatugeukia kwa madaha

“Kumtuliza Salehe yahitaji nguvu ya ziada! Kama ni mganga mwambie wako akuchongee na kishada,” akanipasha! Nisijue alichomaanisha. Nilikuwa naumia ndani kwa ndani. Salehe akanyanyuka haraka na kumfuata Judith ambaye sasa alikuwa anakivuka kizingiti cha mlango na kutoka nje. Salehe akamuwahi akiwa kwenye ngazi pale nje. Nikakimbilia dirisha na kuwachungulia. Salehe akasimama mbele ya Judith aliyekuwa amemalizia ngazi ya mwisho.

“Judy tafadhali! It is over na usiku ule ilikuwa bahati mbaya….na …na unajua hilo, hatukupanga tufanye mapenzi ilitokea tu.”

“Ilitokea tu? Hahahaaaa una kichaa nini?…..yaani uvue nguo mpaka umalize shida zako tena raundi mbili halafu unasema ilitokea tu?” Judith akacheka, akacheka kicheko cha dharau kwelikweli.

“Huwa siachwi, naacha! Na kwako sijakuacha na ndio maana ninapotaka uvue hizo nguo huwa unavua!” akatamba  akizunguka kwa mbwembwe na kusimama mbele ya Salehe.

Sketi yake fupi ilimkaa vyema maungoni, miguu yake minene iliyoshiba urefu wa haja ilikibeba vizuri kiwiliwili cha kike kilichoumbika haswa.

Judith alikuwa mzuri kuliko Raya changanya na ule urefu wa Kitutsi, nilikoma na roho yangu! Pamoja na uzuri wangu wa haja, wenzangu walinizidi uwezo kipesa, hivyo kujiamini kulitoweka!

“Judith haya sio makubaliano yetu….hatuwezi kuoana, hatuwezi kufika popote…na I mean….okay we are done! It is over am your ex now na….am officially dating Zuena,”  Salehe akajieleza polepole akishindwa kupangilia sentensi zake katika mtindo wa kueleweka na mara kadhaa akikatisha maneno na kutafakari cha kusema. Judith akacheka tena, kile kicheko chake kirefu cha dhihaka. Akanyamaza ghafla na kumkazia macho Salehe

“So uliponipigia simu na kuniita hapa ulitaka nimuone Zuena au ulitaka yule kidampa ajue umeniacha au?” akauliza kwa dharau, lakini swali lililokuwa na mantiki kubwa.

“Ulimtukana Zuena kwenye simu na sasa haamini kama wewe ni ex wangu….”

“Na kwanini umuaminishe kitu kisichokuwepo?….kwani uongo hukufanya mapenzi na mimi usiku ule?….yes! nilipokea simu yake na mbovu nikamsemea na wala sikujua ni Zuena nilijua na yule kistuli wako…..mwanamke hachoki kama nzi wamfukuza yumo tu…na mwaka huu tutayaona ya rangi zote.”

“Judith unahitaji kuachana na haya mambo…..it is over!” Salehe akamkemea.

“Unayajua wewe hayo, na kama ulijua ni over usingemsaliti Zuena kijinga namna ile, kwani nilikushikia panga uvue nguo?….naenda zangu na usije ukanipigia simu tena kuniitia ujinga kama huu….na ile kazi yangu niletee kesho mchana niiandikie ripoti.”

“Sikumaanisha hata kidogo hali iwe hivi, ni Raya ndio aliyeharibu kile nilichotaka kukifanya…I am sorry umemjua Zuena kwa njia hii,” akasema Salehe kwa upole.

“Mtajijua! Mpe salamu zangu huyo mke mwenzangu ndani, mwambie mjini hapa cha peke yako sanda, mengine tunashea mpaka makaburi,” Judith akageuka na kuliendea gari lake dogo aina ya Vitz. Akaliondoa, akifunguliwa mlango na mlinzi, akaishia zake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -