Thursday, December 3, 2020

ZUENA BINTI MSASAMBUKO (24)

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ILIPOISHIA jana… “Hashindwi kitu yule wifi, namwamini kwa asilimia zote….Uzegeni hata akitaka mtoto tumboni awe wa Obama na anakuwa, mwanamume ana nguvu ya mizimu sijapataona,” shangazi akamhakikishia mama, Farida akiguna na Subira akicheka kimyakimya, mimi ndio kicheko cha sauti kilinitoka. Shangazi yangu huyu kuna wakati ukimsikiliza unaweza kujiaminisha yasiyoaminika…

SASA ENDELEA..

Farida akajiinua na kuketi akimtazama shangazi.

“Muitoe tu hiyo mimba, cha mno nini kujibebesha mzigo usiokuwa na uhakika nao huyo Uzwegweni sijui ugegeni, anaweza kutuhadaa uko hapa tukaaibika, mtaa huu unaujua shangazi yatazuka ya kuzuka hapa tushindwe kwenda hata gengeni,” Farida akatoa msimamo wake.

Shangazi akalaza kichwa chake upande wa kushoto hali mkono wake wa kulia ukimnyookea Farida na kumwonyesha kiganja chake na vidole vyake vitano. Akamgeukia na kumpasulia…

“Ukoo wa Msasambuko hatutoi mimba… miaka kwa miaka, mimba inatoka kwa kudra za Maulana, mama yenu shahidi tumeshazika watu tayari kwa kutoa mimba, msituletee vilio wakati mlipokuwa mnatanua miguu uko hamkutushirikisha….kesho jihimu mapema tuwahi chole Samvula kwa Uzegeni,” akasonya shangazi akihimiza, akajiinusha toka pale alipokuwa ameketi huku akiuma meno kwa maumivu ya mgongo.

“Wifi nawe unazeeka vibaya hapo tu ushaanza kuuma meno…watoto wa mjini watakusaidia kumtunza baba Hijja…,” mama akamtania wifi yake

“Asaidiwe mara ngapi?’ Farida akachombezea akimtazama shangazi kwa uso wa kusubiria kucheka.

“Mgongo huu ni uzazi tu….nimezaa watoto kumi na moja bila kukimbilia operesheni wala nini na bado nina kitu mnato….we unacho?” shangazi akamwaga radhi akimtupia swali Farida. Tukacheka kwanza tukimtazama shangazi aliyekuwa anafunga vizuri ushungi wake.

“Shangazi una balaa wewe, sasa huo mnato wa kazi gani na uzee huo?” Farida akamtania.

‘Wa kazi gani?….kwani mimi mjane?….mnato wa kumlogea Rama wangu, Baba Hijja mwenyewe nilimkwapua kwa mtu na sasa haibiwi mtu hapa! na uzee wetu huwa tunasukumana ndani mule mpaka panya wanatutazama kwa hasira… raha ile mwenzangu haina ujana wala uzee hasa upate kitu kama hiki cha Mwanaeda’ akatamba shangazi akilitaja jina lake halisi na kutugeuzia makalio yake na kunyonga kiuno chake. Tukapusuka kwa kicheko, bora angekuwa na hayo makalio ya kuringia. Mwenyewe alikuwa mkavu kama gome la mti.

*********

Tuliamkia Chole samvula kule Kisarawe. Safari ilikuwa ya kuchosha ila hatimaye tulifika. Tukaacha basi na kuanza kukatiza kwa mguu, tukiyapita mapori madogo madogo mpaka tulipotokezea kwa huyo Uzegeni. Msururu wa watu waliofuata huduma  ukatufanya tutazamane na shangazi kwanza. Na kujihimu alfajiri yote ile bado tulikuta foleni ya kutosha. Kweli Shida hazina mwenyewe!

Nikitarajia kukutana na mzee wa makamo na haikuwa hivyo. Uzegeni alikuwa kijana tu. Na shuka lake jekundu kiunoni alikuwa amevalia hiziri kubwa mbili zikipishana kifuani kama mkasi. Kichwani alijifunga kaniki nyeusi na uso wake hata sikuuelewa vizuri kutokana na kuchorwa chorwa na vitu vyeupe. Alitisha!

Akapiga manyanga mfululizo akiimba lugha anayoijua mwenyewe kisha taratibu akatulia na kututazama. Akamtambua shangazi

“Karibu mama Hijja, haya za nyumbani’

‘Salama baba, nimekuja na shida ile niliyokwambia jana kwenye simu…na mtoto wa kaka yangu mwenyewe ndio huyu.”

‘Anhaaa! Wala usitie hofu mtwanzi….hapa kazi toka mitondo mbaka mihe shughuli itakuwa imeisha.’ Akatuhakikishia.

Uzegeni akafanya mambo yake, akiyaita maruhani yake na kuzungumza nayo. Habari ndefu hii, alifanya ya kufanya mwishowe nikapewa dawa ya kuoga, kujifusha huku nikiyataja majina wa wanaume ninaohisi wanaweza kuwa wenye mimba na dawa ya kuweka kwenye chai ninayotakiwa kuinywa alfajiri saa kumi na moja  na siku mbili mbele mwenye mimba ningemuona ndotoni. Sayansi ya wenyewe hii , tukalipa elfu 30, tukaondoka,. Shughuli ikaishia hapo!

Nilitimiza yote niliyoambiwa na uzegeni na siku mbili mbele sikumuota hata mama yangu mzazi. Shangazi akapiga simu kwa Uzegeni akiulizia matokeo, akaambiwa tungoje siku saba na niendelee na dawa kama kawaida mpaka zipite hizo siku saba.

*********

Katika kipindi hiki sikutaka hata kuzungumza na yeyote si Salehe si Madobe ambaye sasa alisharejea Buza. Tulikaa na Subira tukipiga hesabu za siku bila mafanikio. Nikaendelea kusubiri kumuota mwenye mtoto bila mafanikio, siku ya saba nikaamka na shughuli ya tumbo! Hali yangu ilikuwa tia maji tia maji, hoi taabani. Nilikuwa navuja damu!

Walinitoa nyumbani wakanipeleka zahanati ikashindikana nikawahishwa Hospitali ya Tumbi. Nilikuwa nalia njia nzima nikitamani  miujiza ya kuniondolea maumivu yale. Salehe alipopata taarifa akaja mbio pale Tumbi akionekana kuchanganyikiwa vibaya mno na asijuwe ninachoumwa.

Wakiwa pale nje wakijadiliana, Salehe alikuwa amesimama mbele ya gari lake akizichezesha funguo za gari  pengine kupunguza mchecheto. Shangazi na mama walikuwa wamekaa kwenye benchi wakiwa wameshika tama, Farida ndio alikuwa amesimama karibu na Salehe wakiongea hili na lile.

Itaendelea Alhamisi

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -