Thursday, December 3, 2020

ZUENA BINTI MSASAMBUKO (27)

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ILIPOISHIA JANA…Niliumia, niliumia sana na safari hii sikuweza kuyazuia machozi yasinitoke. Nimefanya nini hiki? Mtego gani huu? Dhambi gani hii ninayotaka kuichuma mbele ya Muumba kwa kumtendea hivi Madobe. Nikalia kwa kwi kwi nisijali hata watoto walioanza kuamka na kunisogelea pale kitandani…SASA ENDELEA.

Wakatazamana wenyewe kwa wenyewe na wasijue la kufanya. Aisha akanisogelea na kunifuta machozi kwa kiganja chake. “Utapona ma’mdogo usilie,” akanibembeleza, uso wake ukionekana kujaa huruma. Wakanizunguka pale kwa dakika kadhaa wakinitazama ninavyolia. Aisha hakuvumilia naye machozi yakamlengalenga. Hali ile ikanifanya ninyamaze na kutabasamu. Nikamkumbatia huku wengine nao wakinitazama kwa huruma. Nilitamani kuwaambia kueni myaone!

Kulishakucha, wajukuu wakakimbilia kwa bibi yao na kumweleza nilikuwa nalia, mama akaja mbio pale chumbani akiyakusanya matandiko ya wajukuu zake na kuyatupilia kando. Akalifungua dirisha na kuleta nuru angavu mle chumbani. Akaketi kitandani akiikaza vizuri khanga aliyokuwa ameifunga kifuani.

“Haya nini tena mwanangu?” akaniuliza akinitazama kwa upole uliochanganyikana na wasiwasi. Ikawa kama aliniamrisha nikirudie kilio changu upya. Nikalia kwa mengi kwa wakati ule. Mama akanitazama kwa muda kabla ya kunyanyuka kimya kimya na kutoka mle chumbani akiniacha na kwi kwi zangu za kilio.

Nililia kwa dakika kadhaa kisha nikanyamaza na kuketi pale kitandani. Mkorogano wa mawazo kichwani ulifanya nihisi kichwa kikiwa kizito mno, mwili ulipata joto la kutosha kuhisi nilikuwa na homa muda ule. Homa ya mawazo!

Mchana wa siku ile ulinikutia chumbani, nikiwa nimekunywa kikombe cha chai kavu peke yake. Mwili ukiniuma kupitiliza, nikajikunyata kitandani mpaka nilipomsikia mama akiusukuma mlango wa kuingilia mle chumbani na kuingia akiongozana na Subira. Wote kwa pamoja wakaja pale karibu na kitanda na kusimama wima wakinitazama kwa huzuni.

“Nimempigia simu mama Hijja aje tujue cha kufanya maana hapa nawaza na kuwazua sipati kwa alifu wala ujiti,” mama akalalamika akisogea karibu na kuketi pale kitandani, akinipima joto la mwili kwa kiganja chake.

“Lakini Zuena hivi Salehe ni mwanaume pekee katika dunia hii kiasi cha kukuwehusha hivi mwanangu?” mama akauliza kwa masikitiko hali akitikisa kichwa.

“Hujala cha maana tangu jana usiku….unayemlilia yuko huko anashereheka wewe unakufa huku na wahaka,” mama akagongesha viganja vyake na kupiga kofi hafifu hewani. Subira aliyekuwa amesimama naye akaketi chini pembeni ya kitanda akinitazama bila kusema neno. Hali yangu ilimsononesha!

Niliwangoja watimie na wakatimia. Shangazi aliingia jioni saa kumi na mbili. Akanifuata chumbani na timu yake. Akanitazama kwa muda kwanza pale nilipokuwa nimeketi kisha akalipuka na kicheko akiwaacha wenzake njiapanda. Aligundua!

“Ama kweli kenda fumbata si kumi nenda uje kesho….wifi huu mwaka wako wallah!… maana huu ukoo tuna vizazi kama vyura bha!’ akamgeukia mama huku akicheka safari hii kwa sauti kubwa.

“Sasa nini wifi si useme tukuelewe jamani,” mama alishachoshwa na tambo za shangazi. Shangazi akacheka tena cheko refu la kishambenga. Akinyanyuka toka pale alipokuwa ameketi na kusimama katikati ya chumba.

“Safari hii unamjua…uongo?” akanitupia swali akinitolea macho.

“Kumjua nani shangazi?” nikamuuliza moyo ukienda mbio na nusu ya shari nikiiona inakamilika.

“Sasa wifi si utuambie basi tujue tui lipi na maziwa yapi,” mama akadakia wasiwasi ukimjaa kupitiliza.

‘Tena!’ akamjibu kifupi mama akihamisha uso wake uliojaa bumbuwazi toka kwa shangazi na kunitazama mimi ….‘tena?’ akanitupia swali .

‘Mtume Yarabi!’ Subira akahamaki akikishika kifua chake kwa mkono wake wa kushoto. Sikuwajibu wala sikuwatazama sasa, nilijiinamia nikijihisi mkosefu na mpumbavu kuliko wapumbavu wote niliowahi kuwaona duniani. Ukisikia kuchimba kisima na kuingia mwenyewe ndio huku!

Kila mtu akazungumza lake, lawama juu ya lawama, Sasa nikainua uso wangu taratibu na kuamua kuwasukumia jabali zima.

“Ni mzigo wa Salehe…’

‘Kheee!’ wakahamaki kwa pamoja utadhani waliambizana. Shangazi tambo zikimuisha palepale akasimama wima kama nguzo, mama akinikodolea macho utadhani alitaka kuniona kwa saizi kubwa zaidi ya ile aliyoniona, Subira akikikamata kiuno chake utadhani kilitaka kuachana na kiwiliwili chake cha chini. Mtihani niliokuwa nao sasa waliuona, wakausoma na wakaukokotoa na majibu hola! Mhenga aliyesema mchuma janga hula na nduguze hakukosea!

 

Kwa dakika kadhaa tulitembelewa na ukimya kati yetu. Nani aseme nini, kila mtu aliwaza lake na asiliseme. Tukadumu katika ukimya huo mpaka pale shangazi alipopata nguvu ya kuhema kwa sauti na kujitutumua kuongea akitanguliza mguno na kijikofi hafifu hewani.

“Mwenye mimba anaoa, mwenye mke mimba si yake… yahusu!’

“Huyo Salehe anajua una mimba?’ Subira akaniuliza.

“Sijamwambia na sijui hata nikimwambia kama ataniamini,” nikajibu nikimfanya shangazi acheke kwanza.

“Haya mjukuuu mwingine asiye na baba wa kueleweka huyo…. Niliyasema mie wewe na yule mbuzi na kuku, sikueleweka! Katika kuparamia safari hii umeparamia mchongoma kushuka imekuwa ngoma!’ akacheka

‘Shangazi tutafute suluhisho sasa jamani lawama hazijengi ujue,” Subira akaingilia kati.

“…. mmeingia makao makuu ya jeshi na kiroba cha bangi…mnalooo!’ Shangazi akasuta mwenyewe akicheka kana kwamba yale yalikuwa mambo madogo mno akatufanya tutabasamu vile alivyolivuta lile neno bangi na kumalizia na msemo wake. Akatoka mle chumbani akituacha mimi, Subira na mama.

Itaendelea Jumatatu

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -