Wednesday, November 25, 2020

ZUENA BINTI MSASAMBUKO (30)

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ILIPOISHIA JUMANNE…. Madobe alikuwa ameketi  kwenye eneo lilionekana kujengwa kwa ajili ya dirisha lililokuwa limezibwa na nondo. alikuwa ameketi hapo akipishanisha miguu yake, mikono ikiwa imefumbatwa kifuani. Alikuwa akinitazama katika namna isiyotabirika. Alionekana kutulia, uso wake ukiwa umejaa tafakuru nzito. Alikuwa kimya!..SASA ENDELEA…

Nikatamani kumsemesha na nisijue neno la kuanzishia mazungumzo. Nikageuza kichwa changu taratibu na kuwatazama waliobakia. Steve Sikanda! Nikamtolea macho yote nikihisi lile hamaniko likirejea upya, zikazimalizia zile sura mbili zilizobaki, sikuzitambua!

Kwa dakike zile hata ungeniuliza jina langu, sidhani kama akili yangu ingekupa jibu sahihi. Ilikuwa sawa na nusu ya kuchanganyikiwa. Nikamkumbuka Salehe! yuko wapi? nikajiuliza kimoyomoyo.

Mle ndani walikuwa wakizungumza lakini kwa hali niliyokuwa nayo sikuelewa wala sikusikia chochote na wala sikuwapa umakini wowote. Hofu! kitu kibaya sana hiki. Hofu inapofanya kazi kwa umakini huwa inaipumzisha milango yote ya fahamu. Jaribu uone!

“Zuena!” Nikagutuliwa na sauti ya Madobe, alikuwa akitikisa kichwa kwa huzuni ama pengine hasira. Sijui, kwa wakati huu nisingeweza kumtabiria awazacho hata kama angenichekea. Nikamtazama kiunyonge nikizidi kunyong’onyea.

“Una la kusema?” akaniuliza swali muhimu, swali lililogusa hali yangu kwa wakati ule, haya maswali niliyokuwa nikijiuliza na kujijibu mwenyewe, haya niliyokuwa nikiyawaza na kuyawazua yalipewa njia ya kujitokeza hadharani ila ndio vile hofu adui wa haki akanifanya ninyamaze.

Sikumjibu!

Akasimama wima, akijikung’uta vumbi makalioni, bila kuongeza neno akanisogelea na kuchuchumaa mbele yangu. Nilimwogopa kupita maana ya neno ogopa linavyojieleza. Akazidi kunisogelea nami nikaharakisha kuyafumba macho yangu. Nikazibana pumzi kwa sekunde kadhaa na kujizuia kupumua hali midomo yangu ikiumana mithili ya mtu asikiaye uchungu mkali. Akanibusu pajini!

Si busu lile lililofanya nifumbue macho na kuyaangaza tena bali ni sauti ya Salehe ndio iliyonitoa ufahamu kwa mara nyingine tena. Nikageuka haraka na kutazama kulia kwangu. Nikashuhudia Salehe akiingia pale akisukumwa na kuangukia karibu yangu huku akipiga yowe dogo lililoashiria maumivu. Alikuwa amechakaa mno. Nikaduwaa!

Madobe aliyekuwa bado amechuchumaa mbele yangu aligeuka taratibu na kumtazama Salehe. Asionyeshe uso wa huzuni wala furaha. Alikuwa akimtazama kana kwamba alikuwa anaangalia ubao uliodondoka kando yake. Sikumuelewa na hofu yangu ikazidi mara mbili ya mwanzo.

Hakuna kitu kibaya kama kutoelewa dhamira ya adui yako! Hakuna kitu kibaya kama kutojua hisia za mbaya wako, uso wa Madobe ulikuwa mtulivu mno. Hali hii iliniogopesha zaidi. Nadhani kuna mhenga yalimkuta makubwa kiasi cha kugundua Simba mwenda pole ndiye mla nyama! Nina maana yangu kusema hivi kwa vile najua  mcheka kovu hajafikwa na jeraha!

Kana kwamba alitaka niyaone mateso ya Salehe! Alinyayuka toka pale alipokuwa amechuchumaa kusimama kando, akimpisha kijana mmoja aliyemsukuma Salehe pale kando yangu, nikashuhudia Salehe akipokea teke la ubavu lilimfanya alalamike kwa uchungu, mishipa ya shingo ikimkakamaa. Nikapiga yowe kali nikiyahisi maumivu ya Salehe!

“Madobe please….please…..msimuue,” nikamudu kufungua mdomo wangu, viganja vya mikono yangu vikisuguana mbele yake! Ikawa ndio kama nilimwamrisha yule kijana amshindilie Salehe ngumi za uzani wa juu. Nikatambaa haraka nisijali ile sakafu rafu na kumwangukia Madobe miguuni. Nilikuwa nikilia kwa kwikwi nikishindwa kuzungumza katika namna ya kueleweka. Nikamshika Madobe miguu.

“Madobe nakuomba….Salehe hana makosa…. hajui chochote….Madobe nakuomba,” nikatamka nikilia kwa uchungu. Mara kadhaa nikigeuka na kumtazama Salehe aliyekuwa hoi pale chini. Nikaendelela kumsujudia Madobe pale chini nikimlowesha na machozi yangu.

Taratibu akainama na kuniondoa pale miguuni pake. Akiniacha na kusogea kule dirishani na kuketi mkao aliokaa mwanzo. Akapishanisha tena mikono yake na akatabasamu na kutikisa kichwa kisha akaangalia nje, safari hii nikigundua wazi Madobe alikuwa na maumivu makali moyoni na alikuwa akiwaza cha kufanya!

Steve Sikanda akamsogelea, nikukumbushe kitu! Hakuna mtu mbaya kama mpambe! Mpambe huwa ana hisia kuliko hata mhusika. usiwaendekeze wapambe kabla ya kusemezana na moyo wako. Iwe umekosea ama umekosewa jipe nafasi ya kuamua kabla ya kumruhusu mpambe akushurutishe. Mpambe huwa ana nguvu ya ziada na ndio Steve Sikanda. Katika yote yaliyopita masikioni mwangu bila kusikika hili likapita na nikalisikia!

“Muulie mbali unamweka wa nini?…. kwani ulipatana vipi na Judith?” Steve akamshawishi Madobe aliyekuwa bado anatazama kule nje akitikisa kichwa. Nikakurupuka na kusimama na kumvaa Steve Sikanda.

“Judith? …huyu mtu  anahusika vipi na hili?” Nikahoji nikihema kwa kasi.

“Zuena rudi ukakae kule,” Madobe akanifokea.

“Nikae?…. huku mnapanga mauaji?” nikajitutumua nisijue ni kiasi gani nilimtibua Madobe. Akanitolea macho akijiandaa kuongea neno lilionekana kumkwama kooni, akamwemwesa midomo kwa ghadhabu, mishipa ya kichwa ikimsimama na kichwa kutikisika.

“Kaa chini…Pumbavu!” akanikemea kwa hasira nikishuhudia akitetemeka kwa ghadhabu. Akafumba macho na kusikilizia ile hali, mkono wa kuume ukitetemeka na kukunja ngumi huku akivisigina vidole vyake. Alikuwa akiituliza ghadhabu yake!

Niliweweseka na kurudi kinyumenyume, tangu nimfahamu Madobe hakuwahi kuongea kwa sauti kali kama hii, hakuwahi kunionyesha ghadhabu kama hii, hakuwahi kuwa katika hali kama hii.

Nilimuogopa zaidi!

*********

Dakika chache mbele nilimshuhudia Madobe na wenzake wakitoka mle ndani na kufunga mlango kwa nguvu. Nikasikia kufuli likibamizwa nami nikanyanyuka haraka na kumkimbilia Salehe. Nikamgeuza nikijaribu kumkalisha na asiweze! Nikasimama wima katikati ya chumba hiki, nikaangalia kushoto kulikokuwa na dirisha liliwekewa nondo pekee pale alipokuwa ameketi Madobe, nikaliendea dirisha lile na kutazama nje. Hakukuwa na dalili ya njia wala nyumba. Kulikuwa na nyasi ndefu zilizostawi na kufikia robo ya dirisha. sikujisumbua kuufuata mlango, nilijua ulikuwa umefungwa madhubuti!

Nikarejea kujibwaga pale chini kando ya Salehe na ndio nikauona mfuko wa plastiki kwenye kordo. Nikanyanyuka tena na kuufuata. Mfuko ulikuwa na chupa mbili kubwa za maji ya uhai. Nikaichukua moja kwa kasi na kuifungua, nikigeuka na kumuita Salehe kwa furaha kana kwamba nilikuwa nimepata namna ya kutoka mle ndani.

“Amka unywe maji….utapata nguvu angalau,” nikamsemesha nikimuinua na kumpakata. Nikamnywesha maji yale aliyoyanywa kwa pupa kidogo kiasi cha kupaliwa. Nilipatia, dakika chache baadaye aliweza kuketi kwa kujiegemeza ukutani. Mikono yake na miguu ikiwa imefungwa vile vile nilivyomuona mara ya kwanza.” Nikayakusanya matambara niliyokuwa nimefungiwa mimi na kuyatumia kumfuta damu na kumkanda sehemu zilizovimba.

“Watatuua tu,” akasema kwa sauti hafifu akinitazama kwa huzuni. Nikatikisa kichwa kumkatalia nikitoa sauti za mguno kuhitimisha kukataa kwangu.

“Usiwaze hivyo?” nikampa moyo mwenyewe nikiwa na hofu iliyozidi mipaka.

“Zuena” akaita kwa upole nikimeza mate kwa uchungu kidogo na kushuhudia vile vishimo mashavuni kwake vikibonyea. Pamoja na hali yake, uzuri wake haukuchuja!

“Abee!” Nikaitika nikimtazama na kushuhudia akijaribu kutabasamu na kufumba macho kama aliyepata uzito kulitamka alilotaka kutamka.

“Nakusikiliza,” nikamhimiza aseme. Akayafumbua macho yake na kunitazama machoni. Macho yake yenye mvuto wa huba yalipenya  mpaka moyoni yakanifanya nisione michubuko, vumbi wala uchovu aliokuwa nao. Mnaambiwa macho ni madirisha ya moyo na mimi nakwambia macho ni tulizo la moyo wa mtazamaji na hasa abarikiwe macho yanayokwambia karibu kabla ya karibisho lenyewe, yanayokwambia pole kabla ya pole yenyewe, lakini zaidi yanayokufanya upate burudiko na usahau shida na taabu za moyo kwa dakika kadhaa kila uyatazamapo.

Hujawahi kusikia mtu anajiapiza kwa hasira kumzodoa ama hata kumshushia matusi ya nguoni mtu fulani, mwingine akijiapiza kumwacha wake mwandani ama hata kumshushia kipigo lakini huyo anayekusudiwa anapotokeza mbele yake na kumtazama ananywea!. Kumwacha ama kumtaliki mtu kama huyu ni kheri usionane naye, tena umkwepe usitazamane naye hivi hivi utarudi kuniambia hapa. Wenyewe tunayaita wana macho ya Sudi! Wengine wanakwenda mbali na kusema wana macho ya Ibilisi ukimchekea moyo wako anaufilisi! Ndio haya ya  Salehe Masoud. Si mtu anakutazama unajikuta tu unampachika swali “We vipi?”

Salehe alitumia sekunde kadhaa akinitazama tu kabla ya kunishushia fumbo alilokuwa nalo.

“Ni kweli hapo ulipo una mimba yangu?” akalifumbua fumbo lake na kunifanya niukunje uso kidogo na kuangalia pembeni. Sikulitarajia hili swali! Ilikuwa siri, siri yangu na familia yangu.

“Mimba?” nikarudia swali lake

“Yeah…tena ya kwangu,” akamalizia kiuchovu, akisubiria jibu bila kupepesa macho.

“Nani kakwambia hiki kitu?” nikarudishia swali

“Zuena unajua nilikopita kabla ya kuletwa hapa?” akanihoji akitikisa kichwa kwa huzuni.

“Sijui Salehe…lakini nani…”

 

Itaendelea kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -