Saturday, November 28, 2020

ZUENA BINTI MSASAMBUKO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ILIPOISHIA jana …

Haya sasa makubwa ya mzee ubwa, huyu Judith! Nilijua napambana na Raya kumbe Raya mpapai tu, kuna mbuyu huo ulikuwa unangoja wakati ujitokeze. Kumbe kweli alikuwa na ex wake wakifanya kazi na kazi ikazaa kazi katika kazi iliyozua kazi! Kazi kweli kweli.

Haya basi walipitiwa ila ndio watapitiwa mara ngapi na Judith ndio ameshatamba kuwa hamuachi na Raya naye kubembelezwa kule kulimaanisha nini? Naye ni ex au ndio mkulima anajitahidi kupanda mbegu?…. kweli waswahili wanasema ukiona 3 jua kuna mbili zimetangulia! Nilihamanika!

Salehe akarejea ndani akiwa amenyong’onyea kupitiliza. Akasimama mbele yangu ainitazama kwa huzuni. Nilikuwa nimeshajirejesha pale kochini. Akaja polepole na  kuketi kando yangu.  Nilikuwa namtazama tu pasipo kupata hata neno moja la kuvunjia ule ukimya kati yetu. Ningelitoa wapi?

‘Zuena!’ akaniita kwa upole akiniangalia usoni

‘I am sorry!’ Akatamka huku akikishika kiganja cha mkono wangu wa kushoto na kukipeleka mdomoni pake. Akanibusu.

“Najua unajua kila kitu sasa, nimekukosea lakini sikupanga babe  ilitokea bahati mbaya nikajikuta nimelala na Judith, najua nimekukosea najua babe ….na please forgive me!’ akashuka polepole na kupiga magoti mbele yangu. Alikuwa akinitazama kwa huruma. Moyo wangu ulikuwa umepata ganzi kwa dakika kadhaa.  Alinitazama kwa sekunde chache kisha akakilaza kichwa chake mapajani mwangu.

Nilitulia nikiwaza mambo mengi kwa wakati mmoja. Wakati yeye akilala na Judith mimi nililala na Madobe. Nilikuwa mkosaji kama yeye tu isipokuwa makosa yangu hayakuonekana. Lakini kuhusu Judith, kama hajamuacha Salehe ina maana tungeshea mwanaume! Sikuwa tayari!

‘Judith bado anakupenda….kwanini msirudine tu?’ Nikamtupia swali lililomfanya anyanyue kichwa chake na kunitazama kwa mshangao.

“Zuena sina future na Judith!…..okay ngoja nikueleza kwa ufupi’ akanyanyuka toka pale chini na kuketi kando yangu.

‘Familia ya Judith haitaki mtoto wao aolewe na Muislamu tena mwenye asili ya Kiarabu, baba yake Judith na baba yangu hawapatani kabisa kutokana na mambo fulani ya kibiashara na zaidi Judith  hayuko tayari kubadili dini wala kumkosea baba yake….sasa mpaka hapo tuendelee kuwa wote kisirisiri mpaka lini?….kuna future gani hapo?’ akahoji kwa ghadhabu kidogo akionekana kuchanganyikiwa na hali ile.

‘Lakini bado unampenda si ndio’ nikamuuliza mwenyewe nikiomba Mungu jibu lisiwe ndio. Wanawake sisi ni viumbe vya ajabu sana. Tunaweza uliza swali ambalo jibu sahihi tayari tunalo ila tunataka kusikia jibu la uongo ili kuiburudisha nafsi! Sasa uombe Mungu lije la uongo likupumbaze ama sivyo unaweza kupata vidonda vya tumbo!

“YES! Nampenda she is smart na rafiki mzuri anapoamua kuweka mapenzi kando,” akanipa la kunipa. Jibu likaniuma sasa kama anampenda, mimi pale nafanya nini?

“Kwaheri naenda zangu nyumbani,” nikajiandaa kunyanyuka, akanizuia

‘Zuena tatizo lako ni panic! ….sijasema nampenda kimapenzi na sitaki kukudanganya kwa kumkandia Judith ….mwanaume yeyote rijali hawezi kukosa kuvutiwa na Judy but hilo halimaanishi namtaka!’ akajitetea nami nisione tofauti ya kumpenda na kumtaka! Sikumuelewa labda kama wewe umemuelewa unisaidie!

Itaendelea kesho..

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -